Msajili Hazina ataka maboresho Mashirika ya umma - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 20 August 2023

Msajili Hazina ataka maboresho Mashirika ya umma

 

Msajili wa hazina, Nehemiah Mchechu



Mwandishi wetu, Maipac

maipacarusha20@gmail.com


Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ametaka uwepo wa maboresho ya Utendaji katika  Uendeshaji wa Mashirika ya Umma nchini ili kwendana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Wakuu wa Taasisi za Umma na Mashirika wanakutana jijini Arusha kujadiliana Utendaji wa Mashirika hayo ili kuongeza ufanisi mkutano ambao unashirikisha pia baadhi ya mawaziri na Makatibu wakuu.


Akizungumza katika mkutano wa Watendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma unaoendelea jijini Arusha,leo Agosti 19,2023 ,Mchechu amesema lengo la kuwakutanisha Watendaji wa Taasisi za Umma Serikali ni kuboresha Utendaji kazi.


Mchechu amesema, Ofisi ya Hazina imeandaa mkutano huo ambao utakuwa ukifanyika kila mwaka ili kuboresha Utendaji wa Taasisi za Umma lakini pia kuja na mabadilikoa mbayo yataongeza ufanisi na kufikia malengo ya serikali.


"Kikao hiki ni nafasi za kuzungumza changamoto zetu na kujadiliana jinsi ya kuzitatua kwa pamoja kwani taasisi zetu zinamahusiano ya karibu" amesema


Akitoa mada juu ya Utendaji wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Umma, kiongozi wa chama Cha ACT-Wazalendo, ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe amesema kuna haja ya kutungwa upya sheria ya Mashirika ya Umma.


Zitto amesema sheria iliyoanzisha Mashirika ya Umma ina mapungufu lakini pia hakuna sera ya Mashirika ya Umma na ili kuboresha Mashirika ni muhimu kutungwa sheria mpya.


Amesema sheria mpya ya Mashirika ya Umma itasaidia kuleta mungozo jinsi ya upatikanaji Wakurugenzi wa bodi, watendaji wa bodi na masuala ya Hisa , Uendeshaji na mambo mengine muhimu.


Katika hatua nyingine Zitto alishauri Serikali kuunda Shirika Moja la kusimamia hisa za serikali katika Kampuni binafsi ambazo zinakuja kuwekeza nchini.


Zitto alisema hivi sasa Kila Kampuni inayokuja hasa katika madini serikali inalazimika kuunda Kampuni ya kusimamia hisa zake chache hivyo kutakuwa na Kampuni nyingi sana.


"Lakini pia Kampuni ikiundwa tuipeleke kwenye Soko la hisa ambapo watanzania  wengi wataweza kununua hisa "amesema.


Mkutano huo  wa siku tatu unaendeleaje katika kituo cha mikutano Cha Arusha AICC ukiwakutanisha Mawaziri, Makatibu wakuu, watendaji wa Serikali na wajumbe wa bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi zake .





No comments: