KUTOKA MARRAKESH MOROCCO; TANZANIA YAKABIDHIWA uRAIS WA MTANDAO WA JIOPAKI BARANI AFRIKA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 12 September 2023

KUTOKA MARRAKESH MOROCCO; TANZANIA YAKABIDHIWA uRAIS WA MTANDAO WA JIOPAKI BARANI AFRIKA

 




Na Mwandishi Wetu, Marrakesh 


maipacarusha20@gmail.com


Nchi ya Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko kusini mwa jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai, ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) imekabidhiwa u-Rais wa mtandao huo katika kikao cha 10 cha Kidunia cha UNESCO Jiopaki kinachofanyika katika mji wa Marrakesh, Nchini Morocco. 


Ujumbe kutoka Tanzania ulioko Nchini Morocco kupokea heshima hiyo umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu), Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt. Freddy Manongi. 


Rais Mpya wa Mtandao wa Jiopaki Afrika aliyechaguliwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mhandisi Joshua Moshi Mwankunda ambaye ni Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia NCAA.


Faida kubwa ambazo nchi ya Tanzania itazipata kupitia uongozi wa  mtandao huo ni pamoja na;


1. kuongezeka kwa muonekano chanya wa nchi ya Tanzania kimataifa,


2. Kuongezeka kwa idadi ya watalii na watafiti watakaotembelea nchi ya Tanzania kwa Shughuli mbalimbali.


3. Kupanua wigo wa mashirikiano ya kimataifa katika sekta ya uhifadhi na utalii wa jiopaki na miamba (Geopark)


4. fursa ya kuongeza vivutio vingi vya utalii wa miamba kupitia uanzishwaji wa jioapaki mpya nchini Tanzania.



No comments: