MIRIAM ODEMBA FOUNDATION KUJENGA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI MWENDAPOLE KIBAHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 12 September 2023

MIRIAM ODEMBA FOUNDATION KUJENGA MATUNDU YA VYOO SHULE YA MSINGI MWENDAPOLE KIBAHA





 NA: BYARUGABA INNOCENT,  MAIPAC KIBAHA



Taasisi ya Miriam Odemba 'Miriam Odemba Foundation' yenye makao yake Makuu Jijini Dar-eS-Salaam inatarajia kujenga matundu ya choo zaidi ya 40 kwenye shule ya Msingi Mwendapole pamoja na kukarabati jengo chakavu linalosomewa na watoto wa Elimu ya awali ili kuwafanya wanafunzi kufurahia masomo yao

Hayo yameelezwa na Charles Mkoka kwa niaba ya Miriam Odemba alipofika kuitembelea shule hiyo kupata taswira halisi ya uhitaji na gharama zake akiambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mussa Ndomba

Akiwasilisha taarifa ya uhitaji, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rajabu Chalamila amesema jumla ya wanafunzi waliopo ni 1004 wanaotumia matundu matatu tu wakiwemo watoto 90 wa Elimu ya awali

Aidha,Chalamila ameongeza kuwa katika hali ya Kawaida,Shule ilipaswa kuwa na matundu 46 lakini wanapungukiwa na 43 kwani yaliyopo ni 3 tu hivyo nguvu ya haraka inahitajika ili kuwanusuru watoto hasa wa kike na maambukizi ya magonjwa ikiwemo UTI.

"Nawashuru Sana wazazi.Tuliwafuata kuwaomba wameweza kuchangia na kujenga matundu 10 ili kuwawezesha watoto kujisitiri,hata hivyo hayajakamilika na kufanya tatizo kuendelea kuwepo" amesema Chalamila

Akizungumzia upande Walimu,Chalamila amebainisha kuwa nako Kuna shida kwani walimu wa kike wapo 21 lakini wanatumia matundu 2 ya Vyoo na kuhatarisha afya zao

Mwakilishi wa Miriam Odemba Foundation ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kuwaruhusu kufanya kazi ndani ya halmashauri ya Mji Kibaha na kwamba wameona uhitaji,wamechukua picha wataziwasilisha kwa Miriam Odemba ambaye kwa Sasa yupo nchini Ufaransa akiendelea na kazi zake za Mitindo

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwendapole Muhidin Mohamed ametoa salaam za Mtaa na kuipongeza taasisi ya Miriam Odemba kwa kuamua kuanza na Shule ya Msingi Mwendapole. Aidha,ameahidi kutoa ushirikiano muda wowote watakapo hitaji.

No comments: