BENKI KUU YANUNUA KILO 418 ZA DHAHABU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 24 September 2023

BENKI KUU YANUNUA KILO 418 ZA DHAHABU

 



Na Mwandishi Wetu, Geita


maipacarusha20@gmail.com


BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imenunua kilo 418 za dhahabu na kuihifadhi kwenye mfuko wa kuhifadhi dhamana na hifadhi za nchi wa kimataifa uliopo Uingereza.


Dhahabu hiyo inanunuliwa kwa wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa na kabla ya kupelekwa kwenye mfuko wa kuhifadhi dhamana husafishwa kwenye viwanda vilivyopo nchini kikiwemo cha GGR kilichopo mjini Geita chenye uwezo wa kusafisha dhahabu hadi asilimia 99.999 ambayo ni sawa na kutoa dhahabu kwa asilimia 100.


Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini Mjini Geita, amesema benki kuu imeanza kununua dhahabu Septemba 21, 2023.


Tutuba amesema BOT wana dhamana ya kusimamia masuala ya ukuaji wa uchumi na uhumilivu wa bei na mzunguko wa fedha na wa mara ya kwanza toka nchi ipate Uhuru wamekuwa wakitunza akiba ya nchi kwa mfumo wa fedha za nje na kuanzia wameingia kwenye historia ya dunia ya kutunza akiba ya nchi kwa dhahabu inayonunuliwa hapa nchini.


"Benki kuu inatumia nafasi kwenye maonyesho haya kuhamasisha wachimbaji na wafanyabishara wa madini kujua namna watakavyoweza kuuza madini yao kupitia BOT," amesema Tutuba.


Ameeleza kuwa Serikali imefanya maamuzi ya kununua dhahabu ili kuiwezesha nchi kupata fedha za kigeni zitakazowezesha shughuli za kiuchumi lakini pia itakuwa njia mbadala ya kutunza dhamana na akiba ya nchi badala ya kutunza fedha taslimu.


Hata hivyo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko amewapongeza BOT kwa hatua yao ya kununua dhahabu hiyo kilo 418.


"Benki Kuu kununua kilo 400 ya dhahabu kwa bei ya soko ni jambo kubwa mno nawapongeza sana kwa hatua hiyo nafahamu mtaendelea vizuri zaidi," amesema Biteko.



No comments: