KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KIBAHA YAFANYA ZIARA KIGOMA KUJIFUNZA NAMNA YA KUPAMBANA NA HIV-UKIMWI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 9 September 2023

KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KIBAHA YAFANYA ZIARA KIGOMA KUJIFUNZA NAMNA YA KUPAMBANA NA HIV-UKIMWI




 JULIETH  MKIRERI 


MWENYEKITI  wa Kamati ya kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya Mji Kibaha Fokas Bundala ameiongoza Kamati yake kufanya ziara ya Mafunzo Manispaa ya Kigoma Ujiji ili kupata uzoefu wa namna bora ya kupambana na kukabiliana na HIV-UKIMWI kuendelea kuwalinda Watanzania dhidi ya maambukizi Mapya

"Manispaa ya Kigoma Ujiji yenye Kata 19,Mitaa 68 na idadi ya watu 322,524 kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 inashabihiana kwa karibu na Halmashauri ya Mji Kibaha yenye Kata 14,Mitaa 73 na Idadi ya watu 267,000 hivyo kuwa sehemu sahihi ya kujifunzia ili kupata Maarifa mapya " ameeleza Bundala

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha .Mussa Ndomba amesema hali ya maambukizi Kibaha inafikia wastani wa asilimia 5.5 zaidi ya 4.7 ya  wastani wa Kitaifa hivyo kujifunza Manispaa ya Kigoma Ujiji yenye wastani wa 2.9 kutaketa tija ya kupata mbinu mpya zitakazoboreshwa ili ziendane na Mazingira ya Pwani 

Petronila Gwakila,Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji amefurahishwa na ziara hiyo na kwamba taswira nzuri kwa Watanzania kuwa wanafanyakazi vema baina ya Wahe.Madiwani,Kamati na wataalam kwani kati ya Halmashauri 184 nchini,inatia faraja kuchaguliwa kama sehemu ya kujifunzia hivyo ametoa rai kwa kamati kuongeza kasi zaidi.

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI huundwa na Wahe.Madiwani,Wawakilishi wa Madhehebu ya dini,wenye ulemavu,Vijana,Wazee, asasi za kiraia, watu wanaoishi na maambukizi pamoja na wataalamu.

No comments: