WAKILI MADELEKA AACHIWA KWA DHAMANA, ATIMUA MBIO MAHAKAMANI NA KUPANDA BODABODA KUWAKWEPA ASKARI KANZU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 9 September 2023

WAKILI MADELEKA AACHIWA KWA DHAMANA, ATIMUA MBIO MAHAKAMANI NA KUPANDA BODABODA KUWAKWEPA ASKARI KANZU


Wakili Msomi Peter Madeleka akiingia mahakamani


Na Mwandishi Wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


WAKILI wa kujitegemea, Peter Madeleka amelazimika kutimua mbio mahakamani mara baada ya mahakama kumpa dhamana na hivyo kuwaacha polisi wakishangaa .


Staili aliyotumia wakili huyo ni pamoja na kubadili nguo kisha kutoka kwa kasi na kupanda bodaboda iliyokuwa ikimsubiri nje ya lango kuu la mahakama mara baada ya mahakama kuu kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana.




Hayo yametokea leo Septemba 8, 2023 majira ya saa tisa alasiri mara baada ya Jaji, Yohane Masara wa mahakama kuu kanda ya Arusha aliyesikiliza rufaa namba 87/2023 kumuachia kwa dhamana.


Madeleka aliamua kutumia mbinu hiyo baada ya yeye na mawakili wake kuhofia kuwa huenda akakamatwa tena na polisi waliokuwa wamevaa kiraia walionekana ndani na nje ya mahakama tokea majira ya mchana mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kumuachia kwa dhamana.


Wakili huyo ambaye kesi yake inafuatiliwa na wengi akiwa mahakamani alikuwa amevaa shati la bluu lenye mistari meupe ambapo mara baada ya kuachiwa kwa dhamana alitoka nje ya chumba cha mahakama akiwa amefuatana na mawakili wake kisha wakaingia kwenye moja ya vyumba vya mahakama.


Baada ya muda Madeleka alionekana akitoka nje ya jengo la mahakama akiwa kavaa koti jeusi miwani meusi na kofia akitembea kwa mwendo wa haraka hali ambayo haikuwa rahisi kutambulika.




Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Madeleka akitoka mahakamani hapo akifuatiwa na mdhamini wake ambapo walipokaribia lango kuu la dhamana walitimua mbio na bodaboda iliyokuwa karibu na lango kuu kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.


Hata hivyo mawakili wa Madeleka, Boniface Mwabukusi alipoulizwa nini sababu ya hatua hizo, amesema wamelazimika kutumia mbinu hizo alizoziita za kimedani kutokana na hofu huku akionya vyombo vya dola vinapokuwa mahakamani viuache muhimili huo utende kazi zake.




"Lakini ni vema wanapokuwa kwenye maeneo ya mahakama basi waiache mahakama ifanye kazi yake na watu waweze kuona ile sura ya mahakama. Mahakama ni sehemu ambayo inatafsiri vitabu inatafsiri sheria," amesema Mwabukusi.


"Mimi sifurahi, mimi ni mmoja wa watu wanaosikitika sana kuona lundo la watu wanaojaribu kuufanya mchakato wa mahakama kuwa wa kijeshi,"


...Ila najua polisi wetu wana weledi basi watumie weledi kufanya kazi kwenye maeoneo yao na ya wengine wayaache katika sura yake na wanapolazimika kuwepo wajitahidi wawe katika sura inayomwalika kila raia kwenye hilo eneo,".


Kuna wakati kwa kutumia mbinu za medani mtu anaweza kufa kwa kihoro anaweza kuruka dirishani vitu ambavyo si sawa kabisa,".


Awali mahakama hiyo iliporejea majira ya mchana mbele ya Kaimu Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Boniface Semroki Madeleka alitimiza masharti ya dhamana ambapo alisaini dhamana ya shilingi milioni moja na kudhaminiwa na mtu mmoja, Mzambia Amon Kabuje ambaye naye alisaini dhamana ya shilingi milioni moja

No comments: