Lissu azuiwa kuingia hifadhi ya Ngorongoro kufanya mkutano wa hadhara - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 10 September 2023

Lissu azuiwa kuingia hifadhi ya Ngorongoro kufanya mkutano wa hadhara

 




Na: Mwandishi Wetu, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Tundu Lissu umezuiwa kuingia Ndani ya eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kufanya mkutano wa hadhara kutokana na amri ya Polisi



Lissu pamoja na viongozi wa chama hicho, walikuwa wamepanga kufanya mkutano mitatu  Ngorongoro baada ya Jana kufanya mikutano miwili Loliondo.


Hata hivyo wakiwa njiani kwenda Ngorongoro wakitoka Karatu Lissu ma msafara wake walizuiwa baada ya kuelezwa hawana vibali.


Akizungumza akiwa na viongozi wenzake wakati wamefunga barabara kushinikiza waruhusiwe kwenda Ngorongoro, Lissu amesema wameshangazwa polisi kuwazuia kwenda Ngorongoro.


"Tulikuwa tunafata taratibu zote ikiwepo kulipa vibali lakini tumezuiwa na hili jambo hakikubaliki kwani wananchi wa Ngorongoro wanahaki sawa na wananchi wamaeneo mengine Kushiriki katika siasa"alisema


Hata hivyo baada ya kuzuiwa Lissu alihutubia kwa simu na mamia ya wananchi waliokuwa wanamsubiri Ngorongoro na kuwataka wasikate tamaa kutetea Haki zao.


"Dunia unajua kinachoendelea Ngorongoro na mjuwe hampo peke yenu"alisema 


Hata hivyo kamanda wa polisi Mkoa Arusha Justine Masejo alisema walizuiwa mikutano ya hadhara Ngorongoro mwa sababu za kiusalama na kufanya mikutano ni kukiuka sheria.


Alisema watu kadhaa wanashikiliwa kutokana na kukaidi maagizo ya Polisi akiwepo Mwenyekiti wa Chadema Ngorongoro.



No comments: