MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI MITANO YA SHILINGI BILIONI 1.7 WILAYANI NZEGA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 19 September 2023

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI MITANO YA SHILINGI BILIONI 1.7 WILAYANI NZEGA

 




Na Mwandishi wetu, Nzega


maipacarusha20@gmail.com


MWENGE wa uhuru umeanza mbio zake Wilayani Nzega Mkoani Tabora ambapo utakimbizwa kwa muda wa siku mbili kwenye Halmashauri mbili za Wilaya ya Nzega na Mji wa Nzega.


Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Lemeya Tukai, amepokea mwenge huo wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zacharia Mwansasu katika kata ya  Ndala na mkesha utakuwa kata ya Nata.


Tukai amesema ukiwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Nzega chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake mhandisi Appolinary Modest, mwenge wa uhuru utatembelea miradi mitano ya thamani ya shilingi 1,775,767,268.77.


Ameitaja miradi hiyo ni pamoja na huduma za kifedha za Umoja Group kwenye kijiji cha Uhemei kata ya Ndala wa thamani ya shilingi milioni 36 na mradi wa maji Mwakashanhala wa thamani ya shilingi 614,385,268.77.


"Mradi mwingine ni uzinduzi wa shule ya awali na msingi Chief Kabikabo wa vyumba tisa vya madarasa, jengo la utawala na matundu ya vyoo kwenye kijiji cha Kipugala kata ya Puge wa thamani ya shilingi 371,200,000.00," amesema DC Tukai.


Ametaja miradi mingine ni wa mazingira wa shamba la miti katika kijiji cha Ngukumo la shilingi 304,182,000. na uzinduzi wa kituo cha afya Nata cha thamani ya shilingi 450,000,000.


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Abdalla Shaibu Kaim amesema ana imani kubwa na wana Nzega na wataukimbiza mwenge wa uhuru ipasavyo na viongozi kuhakikisha taarifa za miradi na nyaraka zinakuwepo kwenye kila mradi.


Kaim amesema ujumbe wa mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 ni tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai kwa uchumi.



No comments: