NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA
WAZAZI wametakiwa kuwashirikisha watoto katika shughuli mbalimbali wanazofanya ili kuwapa uzoefu na ziwe endelevu hata pale ambapo watakuwa hawapo.
Mbunge wa Kibaha mjini Sylvestry Koka ameyasema hayo aliposhiriki katika mahafali ya darasa la saba shule za Msingi za Kibaha Independent (KIPS), Anex na Msangani ambapo alisema kwa kufanya hivyo ikitokea mmiliki akafariki biashara zitakuwa endelevu.
Koka amesema Sekta binafsi zitaendelea kupewa ushirikiano pale inapohitajika kwani kazi wanazofanya ni kuisaidia Serikali kutoa huduma.
" Sekta binafsi ni muhimu na haina sababu ya kupuuzwa kwani kwa hapa wanaisaidia Serikali kubeba jukumu lamkutoa elimu, na Rais anasisitiza ushirikiano kwa mambo mengi ikiwa nikatika kukabiliana na vikwazo vilivyopo" ameeleza.
Mkurugenzi wa shule za KIPS, Msangani na Anex Yusuph Mfinanga akizungumza katika Mahafali hayo ameahidi kusomesha bure wanafunzi 20 kutoka shule hizo watalaofaulu kwa wastani wa A kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Vuchama na pia atatoa sh. Milion tano kwa mwanafunzi kutoka shule hizo atakayeongoza kitaifa.
Meneja wa KIPS Nuru Mfinanga alisema wanashirikiana vizuri na serikali katika kukabiana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye sekta hiyo lengo likiwa ni kutoa elimu bora.
Nuru amewakumbusha wazazi kuwa karibu na watoto wao kutokana na hali ya sasa ambayo dunia inaenda kasi kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, wawasimamie waendelee kuishi kwa kufuata maadili.
Amesema uwepo wa Sekta binafsi ni moja ya sehemu ya wanaipunguzia mzigo Serikali ambapo pia aliwakumbusha wazazi kuwafuatilia watoto wao badala ya kuacha kazi hiyo ifanywe nanwalimu pekee huku akisisitiza ulipaji wa ada wafanye vizuri kwenye masomo yao na kuwataka walipe ada kwa wakati
No comments:
Post a Comment