Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
maipacarusha20@gmail.com
SHIRIKA la Bandari Zanzibar (ZPC) rasmi limefanya Makabidhiano ya Shughuli na Huduma zote za Uendeshaji wa Bandari ya Malindi kwa Muda wa Miaka Mitano kwa Mwekezaji Afrika Global Logistics kutoka Nchini Ufaransa.
Wakati Majadiliano yakiendelea Tanzania bara juu ya Mkataba wa Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam huku Zanzibar rasmi serikali ya Mapinduzi imekabidhi Huduma na shughuli zote za Uendeshaji wa bandari ya Malindi kwa Mwekezeaji kutoka Ufaransa lengo likiwa kuboresha Ufanisi wa huduma katika bandari hiyo.
Mkataba kati ya Serikali ya Shirika la Bandari na Mwekezaji kampuni ya Afrika Global Lostics ni ya muda wa Miaka mitano ambapo mapato yanayotokana na Bandari hiyo Serikali inachukua Asilimia 30 na Asilimia 70 zinakwenda kwa Mwekezaji.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika hafla fupi ya Utiaji saini na Makabadhiano hayo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Shirika la Bandari Zanzibar Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la hilo Joseph Abdallah Meza amesema lengo la serikali kukabidhi Bandari hiyo ni kuongeza ufanisi na huduma bora.
Amesema kuwa Uwamuzi wa Serikali wa kukabidhi bandari hiyo umezingatia uboreshaji wa Huduma bora za Uwendeshaji na kuwapunguzia wananchi gharama za bidhaa.
"Uwamuzi huu umezingatia mambo mabalimbai ambapo Wenzetu wa Afrika Global Logistic wataboresha huduma na kuondoa changamoto zote ambazo zilikuwepo katika Bandari ya Makontena hapa Malindi," Amesema.
Aidha Amefahamishwa kwamba Mkataba wa awali ulisainiwa Mwezi Mei mwaka huu na Makabidhiano yamefanyika jana Septemba 18 ambapo shughuli zote sasa za uendeshaji wa Bandali ya Makontena itaendeshwa na mwekezaji huyo.
"Baada ya Kuingia makubaliano mwezi Mei mwaka huu na leo hii tumefanya makabidhao sasa shughuli zote zitkuwa chini yao huku tukisubiri Hafla maalum ya Makabidhiano," amefahamisha.
"Uwamuzi huu pia umezingatia kubadilisha tabia za Uendeshaji wa Bandari zetu ambapo sasa tutaongeza taalum na ufanisi wa kazi," ameeleza.
Nae Mwakilishi kutoka Afrika Global Logistic Nicalas Escalin amesema kwamba, ujio wa ni kuongeza Ufanisi katika Bandari Zanzibar kutokana na uwezo wao waliokuwa nao katika uwendashaji wa shughuli za Bandari.
"Ujio wetu ni kuongeza Ufanisi na ubora wa shughuli za Bandari kwani tunaamini AGL imekwa na uzoefu wa muda mrefu katika kutoa huduma bora za Bandari katika mataifa mbalimbali," ameeleza.
Wakati makabidhiano hayo yakiendelea baadhi ya Wafanyakazi wa Bandari ya Majahazi wamelalamikia kupandishiwa kwa ushuru na kuiomba Serikali kuweza kutatua tatizo hilo ambalo limepelekea kushindwa kufanya kazi zao na baadhi ya Bidhaa kuharibika.
"Uwekezaji unauhitaji sana lakini kwa hali napokwenda inatuumiza sisi kutokana na kupadishiwa Ushuru kubwa mkubwa na kupelekea kushindwa kutoa bIdhaa Bandarini,amesema Makame Ibrahim Faki.
No comments:
Post a Comment