TASAF YAPIGA MARUFUKU WANUFAIKA KUTUMIA FEDHA KUOZESHA MABINT - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 22 September 2023

TASAF YAPIGA MARUFUKU WANUFAIKA KUTUMIA FEDHA KUOZESHA MABINT



 NA: MWANDISHI WETU, MAIPAC KIBAHA



WANUFAIKA wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini waliopo chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wameonywa kutumia fedha wanazopata kupitia Tasaf kufanyia sherehe za kuwaozesha mabinti zao wakiwa na umri mdogo.

Meneja ufuatiliaji wa Tasaf Salome Mwakigomba,ametoa kauli hiyo  wakati akizungumza na wanufaika hao waliopo  Kitongoji cha Mwembebaraza katika Kata ya Janga Halmashauri ya Kibaha Vijijini.

Mwakigomba,amewaeleza walengwa hao kuwa kazi ya fedha za Tasaf ni kuziinua Kaya maskini kutoka katika hali duni na kuwa katika hali ya unafuu kiasi cha kuishi kwa kula milo mitatu kwa siku pamoja na kuhakikisha watoto wanakwenda Shule.

Amesema wazazi lazima waweke kipaumbele cha kuwasimamia watoto ili wasome na waachane na tamaduni zilizopitwa na wakati na wanatakiwa kujua Tasaf inatoa pesa ili kuhakikisha watoto wakike wanasoma.

Kwa upande wake Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Pwani Roseline Kimaro, amesema mpango wa kunusuru kaya maskini  unatekelezwa katika Halmashauri tisa zenye jumla ya Vijiji 417 na hadi kufikia Juni ,2023 kaya zinazonufaika na mpango huo ni 35,427.

Kimaro, ameongeza kuwa katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 zaidi ya bilioni 13 zimepokelewa katika madirisha matano na zililipwa kwa walengwa kwa njia ya Taslimu, mtandao na njia ya Wakala.

Hatahivyo,mmoja wa wanufaika wa mpango wa TASAF kutoka katika Kitongoji hicho Ashura Omari, ameishukuru Serikali kwa kuendeleza mfuko wa Tasaf kwani umekuwa na msaada mkubwa kwa kaya maskini.

No comments: