Mwandishi wetu, Babati.
maipacarusha20@gmail.com
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) imewasilisha notisi ya Kukata rufaa kupinga kuachiwa na Mahakama, Wakazi wawili wa kijiji cha Minjingu, wilaya ya Babati mkoa wa Manyara Masiali Lais Kipara(19) na Paulo Richard(23) waliokamatwa na Twiga mdogo, wakiwa tayari wamemuuawa ili kuuza nyama.
Watuhumiwa hao, walikamatwa Februari 14,2023 katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge, (Burunge WMA) na Askari wa wanyamapori, askari wa Burunge na Askari wa Taasisi ya chem chem ambayo imewekeza katika eneo hilo wakiwa na Twiga aliyeuawa mwenye kilo 54.5 mwenye thamani ya sh 35.1 milioni.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki baada ya kusikilizwa kesi hiyo kwa takriban miezi mitano mbele Hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Manyara, Martin Masao aliwaachiwa huru .
Miongoni mwa sababu za kuachiwa huru Watuhumiwa hao alieleza ni kutofautiana kwa ushahidi wa shahidi muhimu katika shitaka hilo,Afisa Wanyamapori wilaya ya Babati Samweli Bayo ambaye alishiriki katika ukamataji wa Watuhumiwa hao.
Hata hivyo ,akizungumza na mwandishi wa habari hizo ,Mwendesha mashitaka wa TAWA, Getrude Kariongi amesema tayari wamewasilisha notisi ya Kukata rufaa.
"Tumepata hiyo Hukumu tunapitia mwenendo wote wa kesi na baadae tutakata rufaa na tuwatoa notisi"amesema
Amesema mapungufu ya kisheria ambayo yamesababisha kuachiwa Watuhumiwa hao wanayafanyia kazi .
Kuachiwa huru Watuhumiwa hao na Mahakamani sasa imekuwa ni awamu ya pili awali waliachiwa na Mahakama kwa madai wana umri chini ya miaka 18 hata hivyo baadae wakakamatwa tena na Polisi na askari wa TAWA na kesi kuanza kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment