NA MWANDISHI WETU MAIPAC, KIBAHA
WATAALAMU wa Ardhi kutoka chuo kikuu cha Ardhi wameendesha Mafunzo ya kuwajengea ufahamu juu ya sheria na usimamizi wa Ardhi kwa Madiwani wakuu wa idara na vitengo, maafisa wa watendaji wa kata na vijiji, wenyeviti wa vijiji na wawakilishi wa mabaraza ya ardhi wa vijiji vyenye migogoro.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Ardhi Fredrick Magina amesema kitendo cha Serikali ya kijiji kugawa Ardhi bila kuangalia mahitaji ya Wananchi, kutokuwa na Mipango ya matumizi ya Ardhi ya kijiji, na Uangalifu Katika kumiliki Ardhi ni baadhi ya visababishi vya migogo ya ardhi.
Magina amesema lengo la mafunzo hayo ni
kutoa Elimu kuhusiana na masuala yanayohusiana na usimamizi wa Ardhi kutokana na kuwepo kwa migogoro ya Ardhi hapa nchini.
Vilevile amesema kutokana na Rasilimali zilizopo ukilinganisha na Ongezeko la mahitaji ya watumiaji hususani kwa upande wa Kibaha , wameona ni vema kuchagua baadhi ya kata, madiwani, watendaji na wajumbe wa Baraza la Ardhi Ili kuwapa Elimu juu ya usimamizi wa Sheria na za Ardhi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Erasto Makala amesema mafunzo hayo yamekuwa mwanga wa kuwasaidia katika Kutoa usuluhishi wa masuala ya Ardhi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Salma Mwalimu amesema Mafunzo waliyoyapata kuhusiana na Ardhi yamewajengea uwezo wa kwenda kutatua migogoro katika sehemu zao za kazi na kuepuka kuzalisha migogoro mipya.
No comments:
Post a Comment