WIZARA YA MADINI KUSHIRIKI MKUTANO WA MADINI MKAKATI UFARANSA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 27 September 2023

WIZARA YA MADINI KUSHIRIKI MKUTANO WA MADINI MKAKATI UFARANSA




Na Mwandishi Wetu


maipacarusha20@gmail.com


Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa umewasili nchini Ufaransa  kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Usalama wa Madini  Mkakati  utakaofanyika kesho Septemba 28, 2023.


Mkutano huo unatazamiwa kujadili masuala muhimu kuhusu madini mkakati, kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili namna ya kushiriki katika kuchochea usimamizi na usambazaji endelevu wa madini hayo.


 Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika  na masuala ya Nishati Safi (International Energy Agency-IEA).


Aidha, mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wafanyabiashara, Wawekezaji, taasisi za kimataifa na taasisi za kiraia.


Mbali na Naibu Waziri, wengine wanaoshiriki kutoka Wizara ya Madini ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, Kamishna Msaidizi wa Madini  sehemu ya Uendelezaji Migodi kutoka Wizara ya Madini, Terence Ngole, Kaimu Mkurugenzi wa Kanzidata kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania ( GST) Hafsa Seif .

VISION 2030:Madini ni Maisha na Utajiri

No comments: