WAWEKEZAJI WAOMBA MABORESHO YA SHERIA NA KANUNI ZA WMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 8 September 2023

WAWEKEZAJI WAOMBA MABORESHO YA SHERIA NA KANUNI ZA WMA

 







Mwandishi wetu, Serengeti 


maipacarusha20@gmail.com


Baadhi ya wawekezaji na Viongozi wa hifadhi za Jamii za Wanyamapori(WMA) wametaka mabadiliko ya sheria na Kanuni za WMA nchini.


Wakizungumza na waandishi wa habari viongozi na wawekezaji hao wamesema bila Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya maboresho WMA zipo hatarini kufa.


Katibu wa Ikona WMA, Yusuph Manyanda alisema WMA nchini zinafanyakazi katika mazingira magumu na baadhi zimeanza kushindwa kujiendesha kutokana na sheria zilizotungwa miaka ya karibuni.


"Miongoni wa changamoto ni kupata fedha za uendeshaji kutokana na fedha wanazokusanya kupelekwa Hazina na kuchelewa kurudishiwakatika WMA"alisema 


Alisema fedha zilizokusanywa kuanzia mwezi January mwaka huu hadi sasa hawajapata mgao wa fedha na hii ni kwa WMA zote nchini.


"Mara ya mwisho kupata fedha zetu ni mwezi wa nne ambapo tulipata pesa za mwaka Jana, hizi fedha ndio tunategemea kufanya doria kulipa mishahara na matumizi yote hivi kama hatuzipati kwa wakati na hatuna ruzuku imekuwa shida kubwa kwetu"amesema


Alisema tayari changamoto hii wameifikisha Wizarani,bungeni Hadi kwa Mawaziri lakini hakuna ufumbuzi.


Katibu wa Makao WMA, Jeremiah Bishoni amesema wamefatilia suala la fedha lakini wameambiwa yafanyike mabadiliko ya sheria ya fedha ndipo suala lao lipate ufumbuzi.


"WMA zipo katika hali mbaya ni chache ambazo zinapata fedha tofauti na za watalii wanaotembelea hifadhi zao ndizo walau zinajiendesha"alisema



Mwekezaji anayemiliki hoteli na kambi za kitalii kadhaa katika maeneo ya WMA, Wilbard Chambulo anasema Serikali inapaswa kuboresha sheria na kanuni za WMA .


Chambulo anasema licha ya kuchelewa kupatiwa fedha lakini pia kuna shida kubwa ya sheria na Kanuni ambazo zinazuia wawekezaji kuwekeza katika maeneo hayo.


"Kuna hili jambo la kutakiwa kusaini mikataba mipya Kila mara hili ni tatizo kwani utakuta Mwekezaji anaweka miradi mikubwa na baada ya muda anatakiwa kusaini mkataba kuendesha eneo lake Sasa hakuna Usalama wa uwekezaji kwa sababu anaweza kupewa mtu mwingine eneo lako"alisema


Alisema Mwekezaji makini anataka kukaa muda mrefu kwenye eneo alilowekeza na kuna usalama wa uwekezaji wake, lakini kwa kanuni za WMA kila baada ya muda mfupi unapaswa kusaini mikataba ya kuendelea kuwekeza na ikitokea baadhi ya viongozi wa WMA kushawishiwa na mwekezaji mwingine basi wanaanzisha mgogoro kukuondoa eneo ambalo umelitunza sasa hii sio sawa"anasema


Chambulo anasema katika WMA pia kuna changamoto ya baadhi ya viongozi kutokuwa wahifadhi na hivyo hujali maslahi yao kuliko uhifadhi hatua ambayo imekuwa ikichangia migogoro .


“Baadhi ya viongozi wamekuwa na changamoto, ikiwepo kutoshirikisha wawekezaji katika bajeti, kutopeleka fedha vijijini na kuingiza mifugo maeneo ya hifadhi na kushindwa kuzuia vitendo vya ujangili na uharibifu wa hifadhi”anasema.


Chambulo alitolewa mfano eneo la Burunge WMA ambapo kuna uvamizi mkubwa wa maeneo ya uhifadhi ikiwepo Mifugo na uvuvi haramu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.


Joseph Laizer mkazi wa Minjingu katika eneo la Burunge WMA,ameitaka serikali kutazama muundo wa WMA ili uweze kusaidia uhifadhi, Utalii na kusaidia Jamii iliyotoa ardhi.


"Hatuoni faida ya WMA wamechukuwa maeneo yetu fedha za Utalii hazitumwi vijiji kwa wakati kama zamani lakini pia kuna migogoro mingi na wawekezaji ambayo inapaswa kutatuliwa "alisema.


Kuna maeneo ya WMA 38 nchini ambayo yametolewa na wananchi ili kuendeleza uhifadhi na Utalii ambayo yapo pembezoni mwa hifadhi za Taifa na mapori ya akiba.



No comments: