WAZIRI MAVUNDE AMPONGEZA MWEKEZAJI MZAWA BLUE COAST - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 29 September 2023

WAZIRI MAVUNDE AMPONGEZA MWEKEZAJI MZAWA BLUE COAST

 



Na Mwandishi wetu, Geita. 


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI wa Madini, Anthony Peter Mavunde ameipongeza kampuni ya Blue Coast iliyofanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya madini.


Blue Coast ni kampuni ya kizawa inayojishughulisha na usafirishaji wa bidhaa na mizigo ya aina zote kwa zaidi ya miaka 20 ndani ya Tanzania, Afrika Mashariki na kati na kusini mwa Afrika.


Pia, Blue Coast inasafirisha aina mbalimbali za bidhaa vimininika na bidhaa yabisi mfano mafuta ya petroli, diizeli, makaa ya mawe, cement na vinywaji mbalimbali.


Waziri wa Madini Mavunde, akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya Blue Coast amesema Mwenyekiti wa makampuni mzee Athanay Inyasi amefanya kazi kubwa ya kusimamia Blue Coast hadi kufikia hatua hiyo.


Amesema uwekezaji wa kampuni hiyo umesaidia kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania na kuchangia mapato ya halmashauri na  kodi ya Serikali hivyo uwepo wake una maana kubwa katika maendeleo ya nchi na hususani mkoa wa Geita.


Hata hivyo Waziri Mavunde amewataka wafanyabiashara, wachimbaji na wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi ili kuomba zabuni.


"Kwa hiyo nitoe rai kwa makampuni mengine yakitanzania kuchangamkia fursa hii sisi kama Serikali tutahakikisha tunaisimamia sheria hii ya local content vizuri ili watanzania wengi  zaidi waweze kunufaika kwani tunahitaji kuwaona  akina mzee Inyasi wengi zaidi kama alivyomsema RC m ili mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini  katika maisha ya watanzania na kupitia uchumi huu tuweze kukuza pia uchumi wa nchi na jambo hili linawezekana," amesema Mavunde.


Mwenyekiti wa makampuni ya Blue Cost  Athanas Inyasi amesema uwepo wa sheria ya watoa huduma au maudhui ya ndani (local Contect) imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania, huku ajira 500 zikitolewa na kampuni hiyo.


"Ninamshukuru kwa namna ya pekee Rais wetu Dkt  Samia Suluhu Hassan anavyoendelea kutuwekea mazingira mazuri sisi wafanyabiashara na wananchi wote  kwa jumla na mambo yetu yakaweza kuendelea kukua kitaifa na kimataifa," amesema Inyasi.


Mkurugenzi mtendaji wa Blue Coast, Ndahilo Athanas amesema kampuni yao imejikita pia katika kujenga miundombinu ya maendeleo kama madarasa na madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo Geita wakiwa na lengo lakuangalia na sekta nyingine hasa sekta ya afya kwa siku chache za mbeleni.


"Mheshimiwa Waziri kwa kuzidi kutambua umuhimu wa sekra ya elimu  kampuni yetu imetoa mchango wa shilingi milion 150 kupitia mfuko wa GPE Multplier Grant kwa ajili ya uboreshaji wa elimu katika shule za msingi yenye lengo lakutatua changamoto za walimu nchini," amesema Ndahilo.


Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji kuboreshwa inasababisha kuwatengeneza mzee Inyasi wengi zaidi kwani ajira alizotoa ni nyingi.


"Mzee Inyasi ametoa ajira zaidi ya 500 ikiwemo wana Geita 360 nitumie nafasi hii kuwataka wachimbaji wadogo pindi wanapopata fedha waweze kuwekeza katika biashara ili kuwaongezea kipato," amesema Shigela.


Mwenyekiti wa makampuni ya Waja, Chacha Mwita Wambura, ambaye ni mjumbe wa NEC viti 20 Tanzania Bara, amempongeza mzee Inyasi kwa uwekezaji mkubwa alioufanya Geita.


"Mzee Inyasi amefanya mambo makubwa Geita kwa kutoa ajira na kusababisha maendeleo kwa mji wetu wa Geita," amesema Wambura.



No comments: