Chemchem kugawa baiskeli za walemavu zaidi ya 300 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 6 October 2023

Chemchem kugawa baiskeli za walemavu zaidi ya 300

 


Mkurugenzi wa chemchem association Fabia Bausch akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi baiskeli


Mwandishi wetu. Babati

maipacarusha20@gmail.com


Taasisi ya Utalii ya chemchem ambayo imewekeza wilaya ya Babati mkoa wa Manyara imeanza kugawa  Baiskeli bure kwa Watu wenye ulemavu wa miguu zaidi ya 300 mkoani Manyara ili ziwasaidie kufanya shughuli za kiuchumi.


Baiskeli hizo, zenye thamani ya zaidi  shilingi milioni 45 zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Weelchair Fondation, kupitia Taasisi ya chemchem association ambayo ipo chini ya Mwekezaji mwa shughuli za Utalii na uhifadhi katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii ya Burunge wilaya ya Babati.


Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo  kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen  Sendiga, kwa walemavu, ambao wanaishi katika vijiji vinavyounda hifadhi ya eneo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Burunge alipongeza Chemchem kwa msaada huo.


Twange  aliwataka wananchi wa mkoa wa Manyara, kuendeleza uhifadhi wa mazingira ili kuvutia watalii na wawekezaji kutoa misaada zaidi.


Alisema msaada wa Baiskeli hizo ni ishara ya mahusiano mazuri baina ya wananchi na mwekezaji wa Chemchem katika eneo hilo, kwani pia amekuwa akitoa misaada katika sekta nyingine, ikiwepo elimu, Afya na Maji.


"Nawaomba tuendekeze mahusiano haya mazuri ili tupambane na matukio ya ujangili katika eneo letu ili tuvutie watalii zaidi ambao wataleta fedha ambazo zitaendelea kugawanywa vijiji 10 vinavyounda Burunge WMA"alisema


Alisema Baiskeli hizo zisaidiwe wenye ulemavu kuweza kushiriki vyema shughuli za kiuchumi na kujiletea maeneo.


Naye Mkurugenzi wa Chemchem Association, Fabia Bausch alisema wanajivunia uwepo wa mahusiano mazuri na jamii na ndio sababu wataendelea kutoa misaada mbalimbali kusaidia kijamii.


Alisema licha ya msaada huo wa Baiskeli pia wanaendelea kusaidia pia makundi ya akina mama kujikwamua kiuchumi kwa kupewa fedha na elimu ya ujasiriamali,kusaidia vita dhidi ya ujangili na wamesaidia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi.


"Tumekuwa tukisaidia miradi ya elimu,maji Afya lakini pia kuwasaidia akina mama kushiriki vyema katika Utalii"alisema


Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa Baiskeli hizo, Maria Haido alishukuru taasisi ya chemchem na Serikali kufanikisha kupatiwa Baiskeli na kuahidi sasa ataweza kutoka nyumbani na kwenda kujitafutia mahitaji yake kwa urahisi.


Meneja miradi wa Taasisi ya  Chemchem association,Martin Mng'ongo alisema wanatarajia kugawanya zaidi ya Baiskeli 300 mkoani Manyara na maeneo mengine yenye uhitaji.


"Leo tumeanza kutoa Baiskeli  kwa baaadhi ya wenye ulemavu wanaoishi vijiji vilivyopo ndani ya Burunge WMA, ikiwa pia ni sehemu ya uzinduzi wa tamasha la chemchem 2023 na tutaendelea kutoa Baiskeli maeneo mengine"alisema.


Eneo la Burunge WMA lipo kati kati ya hifadhi za Taifa za Tarangire na Manyara ambapo kuna idadi kubwa ya wanyama hasa Twiga hata hivyo, kumekuwepo matukio ya ujangili wa Twiga kwa ajili ya kitoweo.


Hata hivyo,katika.siku za karibuni kumekuwepo na operesheni kubwa za kuwasaka majangili kwa kuhusisha kikosi Maalum Cha Mamlaka ya wanyamapori (TAWA) askari wa Burunge WMA na Askari wa chemchem na majangili kadhaa wamekamatwa.



No comments: