Macklion yatwaa tena ubingwa Chem chem Cup, 2023 yazoa million 2.5 na Kombe - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 31 October 2023

Macklion yatwaa tena ubingwa Chem chem Cup, 2023 yazoa million 2.5 na Kombe

 



Mgeni Rasmi Afisa michezo Mkoa Manyara alimkabidhi kikombe nahodha wa timu ya Macklion baada ya kutwa Ubingwa wa chemchem CUP 2023


Mkurugenzi wa chemchem Association Nicolas Negri akizungumza na wanamichezo pamoja na mashabiki wa soka waliojitokeza uwanjani hapo


Mwandishi wetu, Babati


maipacarusha20@gmail.com


Timu ya Macklion FC imetwaa kwa mara ya tatu mfululizo ubingwa wa mashindano ya Chem chem Cup mwaka 2023 baada ya kuitandika mabao 2-0 Macedonia FC katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Mdori uliopo wilayani Babati mkoani Manyara.


Katika michuano hiyo ambayo mwaka huu ilikuwa imeshirikisha timu 33 lengo lake ni kupiga vita ujangili wa Twiga katika eneo la vijiji 10 ambavyo vinaunda Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge, wilayani Babati mkoa Manyara.


Mbali na timu hiyo ya Macklion kutwaa ubingwa pia ilishuudiwa Maweni FC ikitwaa ubingwa kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18 baada ya kuikung’uta Mwada mabao 2-0.


Kwa Upande wa timu za Wasichana  Mwada Queens ilitwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa mabao 4-0 Maweni Queens .


Wachezaji Bora kwa Upande wa timu za wakubwa,vijana na wasichana walipewa zawadi za vikombe, kiatu Cha Dhahabu na mkono wa dhahabu kwa makipa Bora.


Mchezo wa fainali ukiendelea


Akifunga mashindano hayo afisa michezo Mkoa wa Manyara, Pastory Samwel kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa Arusha, amewapongeza wandaaji wa mashindano hayo taasisi ya Chem chem kwa kutoa elimu ya uhifadhi kupitia michezo lakini pia kupambana kuhakikisha Soka linaendelea kuchezwa.


Amesema mashindano hayo chini ya kauli mbiu ya Okoa Twiga imekuwa ni daraja kwa vijana kuweza kutimiza ndoto zao kwani wapo ambao wamepita hapo na sasa wanacheza Ligi Kuu akiwemo kiungo wa Ihefu FC, Yusuph Athumani.


“Afcon ya mwaka 2027 itachezwa hapa Tanzania na Mkoa jirani wa Arusha mechi zitachezwa hivyo kwetu itakuwa ni fursa kwa uwanja wetu huu bora wa Mdori kupata nafasi ya timu kufanyia mazoezi”, amesema Samwel.


Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya Chem chem, Nicolaus Negri ameweka wazi kuwa wametumia Tsh99,220,000 kuendesha mashindano hayo ambapo pia wamefanikiwa kutao elimu juu ya uhifadhi wa wanyamapori katika eneo la hifadhi ya jamii ya Burunge.


“Dhumuni letu ilikuwa ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira, kutoa elimu kwa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira, kupiga vita ujangili wa wanyamapori, kujenga mahusiano katika jamii pamoja na kuibua vipaji”,amesema Negri.


Kwa upande wa zawadi timu ya Soka kwa wakubwa bingwa amepata Tsh2,500,000,mshindi wa pili Tsh1,500,000,mshindi wa tatu 1,000,000,Wanawake bingwa Tsh1,500,000,mshindi wa pili Tsh1,000,000,mshindi wa tatu Tsh500,000,.


Vijana U-18,bingwa amepata Tsh1,000,000, mshindi wa pili Tsh600,000, mshindi wa tatu Tsh400,000 pia kulikuwa na zawadi za medali, kiatu cha Dhahabu kwa mfungaji na mchezaji bora lakini pia Gloves za Dhahabu kwa Kipa bora.


Mashindano hayo yamefanyika kwa mwaka wa Nane sasa tangu yalipoanzishwa mwaka 2014, ambapo yalishirikisha timu 33 za Mpira wa miguu za wakubwa,Vijana U-18 na wanawake kutoka vijiji 10 vya jumuiya ya hifadhi ya Wanyamapori Burunge.


Afisa Wanyamapori wilaya ya Babati, Laizer alisema halmashauri ya wilaya ya Babati inapongeza chem chem kutumia michezo katika Kupambana na ujangili.


Laizer alisema tangu kuanza kwa mashindano hayo wananchi wengi wamejua faida ya uhifadhi na Kupambana na ujangili.


"Tunawaomba wawekezaji wengine kuiga chemchem katika kuwashirikisha watu wengi katika uhifadhi"alisema




Katika fainali hiyo Taasisi ya chem chem pia iliendelea kutoa msaada bure wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu.


No comments: