KIJANA AIBA SAKRAMENTI YA EKARISTI KANISANI IFAKARA AKAMATWA AKITOROKA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 28 July 2024

KIJANA AIBA SAKRAMENTI YA EKARISTI KANISANI IFAKARA AKAMATWA AKITOROKA

 

Kijana mkazi wa Ifakara Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro Enock George Masala anayedaiwa kuiba sekrament kanisani

Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo la Ifakara Padre Marcus Mirwatu


Na: Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


LEO ni Jumapili siku ambayo wakristo wa madhehebu mbalimbali huenda kanisani kwa ajili ya kuabudu, kuna wengine wanaingia wakiwa na malengo tofauti ikiwemo kuiba.


Kijana mmoja mkazi wa Ifakara Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro Enock George Masala (19) amekamatwa wakati akijaribu kutoroka na Sakramenti takatifu baada ya kukomunika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Andrea Jimbo Katoliki Ifakara.


Kijana huyo alikamatwa na walinzi wa Kanisa hilo wakati Misa ya kwanza ya Asubuhi Julai 28 ikiendelea, na kutangazwa ndani ya kanisani kwa tukio la wizi wa Sakramenti hiyo aliyotaka kutoroka nayo.


Paroko wa Kanisa kuu la Mtakatifu  Andrea Jimbo la Ifakara Padre Marcus Mirwatu alisema kumekuwa na wimbi la matukio ya watu wasio wakatoliki wanaongia Kanisani kukomunika kisha kuondoka na Sakramenti kinyume na taratibu na miongozo ya Kanisa hilo.


Kiongozi huyo wa Kanisa alilaani vitendo hivyo na kuagiza wakisto kuwafichua watu hao, wanaokwenda kinyume na Imani ya Kanisa hilo, huku akiwataka walinzi wa Kanisa kuendelea kumuhoji kijana huyo ili kufahamu sababu za kijana huyo kufanya tukio Hilo.


"Tunashindwa kuelewa watu Hawa wanatumwa na nani kufanya vitendo hivi, hatuelewi Wana malengo gani kwa Kanisa letu, hivyo ninaomba kijana huyu aendelee kuhojiwa kwanini amefanya tukio hilo" alieleza Paroko Padre Mirwatu.


Aidha kijana huyo Enork Masala alipohojiwa na mwandishi wetu alikiri kuwa yeye si Mkristo Mkatoliki, na kwamba alitenda tukio Hilo baada ya kuona Wakristo wengine wakipanga foleni na kupokea Sakramenti, hivyo hakujua kama ni kosa kuondoka nayo Kanisani hapo huku aiweka bayana kuwa hakuna taratibu zote za kikanisa anazozifahamu.


Mwisho

No comments: