RAIS SAMIA AZINDUA MITAMBO YA UCHORONGAJI MADINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 22 October 2023

RAIS SAMIA AZINDUA MITAMBO YA UCHORONGAJI MADINI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua mitambo ya uchorongaji madini pambeninyake ni Waziri waadini Anthony Mavunde

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa  Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua mitambo ya uchorongaji madini 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 


maipacarusha20@gmail.com


Zaidi ya Shilingi bilioni 9.2 zatumika kununua mitambo STAMICO


Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa  Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  leo Oktoba 21, 2023 amezindua  Mitambo Mitano (5) ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo pamoja na vifaa kazi vingine vya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) vyenye jumla ya thamani ya shilingi 9,178,559,128.


Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Mkutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma  ambapo umeenda sambamba na kukabidhi vifaa hivyo kwa wachimbaji  Wadogo wakiwemo Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) ambapo  vinajumuisha Mitambo  Mitano ya uchorongaji  yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.22.  


Vile vile, Vifaa vingine ni pamoja na Lori tatu za kubeba vifusi vya madini (Dump trucks) zenye thamani ya Shilingi milioni 544, Lori moja la kubeba mitambo (Lowbed) lenye thamani ya Shilingi milioni 274, Mtambo mmoja wa kusaga makaa ya mawe (Coal crusher) wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.58.


Vifaa vingine ni Mtambo mmoja wa kusaga miamba kwa ajili ya kokoto (stone/aggregate crusher) wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.137, Mtambo mmoja wa kufua upepo yaani Air compressor wenye thamani ya Shilingi milioni 424, Lori moja la kubebea maji (water bowser) lenye thamani ya Shilingi milioni 210.


Aidha, Mitambo miwili ya uzalishaji wa Mkaa Mbadala (Rafiki Briquettes) wenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.396, Magari mawili (2 hardtop) kwa ajili ya shughuli za uzalishaji madini migodini yenye thamani ya Shilingi milioni 317 na Jaw Crusher 10, Metal Detector (20) na Injini ya Dizeli aina ya 24HP Moja (1) vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 72.5.








No comments: