MWANDISHI WETU, MAIPAC KIBITI
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke amesema hatakubali kuwepo kwa migogoro na badala yake atasisitiza mshikamano kuleta maendeleo kwenye chama na kwa wananchi.
Ndaruke amesema Chama hicho kinalenga zaidi kuendelea kuleta maendeleo kwa kutekeleza miradi inayokwenda kumaliza kero za wananchi na hakina nafasi ya kutengeneza migogoro.
Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa Kata ya Bungu uliofanyika kwa lengo la kuelezea namna ilani ilivyotekelezwa sambamba na kufanya harambee ya ujenzi wa ofisi.
Katibu wa CCM Kata ya Bungu Hussein Tinge amemshukuru Serikali kwa namna inavyopeleka miradi na kuleta mabadiliko ya Maendeleo katika kata hiyo.
Tinge amesema ofisi wanayotarajia kuijenga gharama yake ni zaidi ya Miln 13 na kwamba itakuwa sehemu ya kitegauchumi kwa kuwa na vyumba vya biashara vya kupangisha.
Tinge amesema Chama hicho kitasimamia kwa uadilifu michango inayotolewa na wanachama na wadau mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo kwa kutoa mrejesho wa kila hatua.
No comments:
Post a Comment