Na: Mwandishi Wetu- Dar es salaam
maipacarusha20@gmail.com
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Philip Isdory Mpango amesema kuwa usafiri wa anga ni kichocheo kikubwa cha kukuza Sekta ya Utalii na kuongeza pato la Taifa nchini.
Mhe. Mpango ameyasema hayo leo tarehe 03 oktoba, 2023 wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya ATCL aina Boeing 373 Max-9 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam.
Mhe. Mpango aliongeza kuwa ili tuweze kufikia lengo la watalii milioni tano na mapato yatokanayo na utalii dola za kimarekani milioni 6,000,000 lazima kuwepo na usafiri wa anga wa uhakika.
Vilevile, akitoa takwimu ya ongezeko la abiria nchini alisema kwamba kwa mwaka wa fedha 2016/17 abiria waliotumia shirika la Ndege la ATCL walikuwa 161,380 hadi Abiria 1,073,400 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 huku akifafanua kuwa ongezeko hilo pia lilichangiwa na ongezeko la watalii kutoka nje waliokuwa wakitumia usafiri wa ndege ya ATCL.
Ujio wa Ndege hii ya Beoing 737-Max 9 kutaifanya ATCL kufikisha ndege 5 za masafa ya kati na hivyo kutaongeza idadi ya wasafiri ambao wataunganisha safari zao hapa JKNIA ambapo tutaanza safari za masafa marefu kama vile kwenda London nchini Uingereza mwaka ujao wa fedha.
Katika sherehe hizo, walishiriki viongozi mbalimbali wa serikali ikiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Naibu wake Mhe. Dunstan Kitandula(Mb).
No comments:
Post a Comment