MAONYESHO YA TATU YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA 2023; KUFANIKA MKOANI ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 20 November 2023

MAONYESHO YA TATU YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA 2023; KUFANIKA MKOANI ARUSHA

 



Na Elinipa Lupembe, Arusha


maipacarusha20@gmail.com



Maonesho ya tatu ya wiki ya Huduma za Kifedha Kitaifa 2023, yanafanyika mkoani Arusha, kuanzia kesho, kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abed Jijini,  Arusha.


Akizungumza na Wandishi wa Habari leo, Kamishna wa Idara ya Uendeshaji Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, amesema kuwa Maonesho hayo yatafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 20 - 26 Novemba, 2023 na kuwataka wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani, kufika kwenye maonesho hayo.


Amesema kuwa lengo la Wiki ya Huduma za Kifedha ni kutoa elimu kwa Umma, juu ya Huduma za kifedha na kuwa na uelewa kuhusu matumizi sahihi ya huduma rasmi za kifedha, zitakazosaidia katika kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.


"Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 - 2029/30, Elimu kwa Umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo" Amesema Dkt. Mwamwaja


Ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuboresha mazingira rafiki ya huduma za kifedha, na mpaka sasa asilimia 53.8 ya watanzania hutumia huduma rasmi za kifedha, ikiwa bado idadi kubwa ya watanzania hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha, hivyo utoaji wa elimu kwa Umma utasaidia, wananchi kuacha kutumia mifumo isiyo rasmi ya kifedha na kufikia lengo la Serilaki la asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.


Naye Meneja msaidizi wa Mawasiliano, Benki kuu ya Tanzania, Noves Mosses, amesema Benki  hiyo ni msimamizi wa taasisi zingine za kifedha, iliyojikita kutoa elimu kwa Umma, ili kuwa na uelewa mpana kwenye masuala ya huduma za kifedha ili  kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.


Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi

kutembelea kwenye mabanda, yaliyopo kwanye Uwanja huo wa Maonesho na kuwasisiza, wananchi wenye wenye changamoto au kuhitaji kupata ufafanuzi na utatauzi wa changamoto hizo, kwa kuwa huduma zote zitatolewa bure, 

 

Kwa upande wake Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika,  kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika mko wa Arusha, Grace Msambaji, amesema vyama vya ushirika humwinua mnyonge kutoka chini, na kuwa wamejipanga kuwahudumia wananchi katika kuendeleza uchumi wa watanzania.

No comments: