MFUMO WA iMES UTAONGEZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI KATIKA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA SERIKALI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 10 November 2023

MFUMO WA iMES UTAONGEZA UWAJIBIKAJI KWA WATUMISHI KATIKA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA SERIKALI

  



Na Elinipa Lupembe, Arusha 


maipacarusha20@gmail.com



Imeelezwa kuwa, ikiwa mpango wa Serikali wa kutumia Mfumo Jumuishi wa Kutathmini Utekelezaji wa shughuli za Serikali ( iMES), ukisimamiwa vizuri, utawezesha watumishi kufikia malengo ya Serikali, ya kutoa huduma bora kwa wananchi, kwa kuwa mfumo huo unauwezo wa kuonesha hatua za utekelezaji wa shughuli zote za Serikali hatua kwa hatua.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, wakati akifunga mafunzo ya mfumo huo kwa Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa kwa usimamizi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI.


Mhe. Mongella amesema kuwa mfumo huo, ukitumika kwa weledi,  utampa kila msimamizi wa mradi kutekeleza majukumu yake bila kusukumwa na kusaidia miradi kutekelezeka kwa wakati na kukamilika kwa ufanisi na kwa mafanikio makubwa.


Hata hivyo, Mhe. Mongella, amewataka wakurugenzi wa halmashauri, kuwajengea uwezo watendaji wa chini wanaohusika katika usimamizi wa miradi, wakiwemo Walimu na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji, ili kuwa na uelewa wa pamoja wa kuhakikisha mfumo wa iMES unafanyakazi kwa weledi na kufikia malengo ya serikali.


Aidha, ameipongeza Ofisi ya Rais TEMISEMI kwa kuja na mfumo rahisi wenye gharama nafuu, ambao utaondoa tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, huku ukimsukuma kila mtumishi kuwajibika kwa nafasi yake kwa kuwa mfumo huo, unaruhusu kupima na kutathmini hatua zote za utekelezaji wa mradi.


"Mfumo huu unawapa nafasi Wakurugenzi kusimamia shughuli zote kupitia mfumo na kufahamu hatua zote za utekelezaji wa mradi kama unachelewa kuweza kuchukua hatua na kutambua ukwamishaji umefanywa na idara gani, mfumo umerahisisha kazi lakini unambana kila mtumishi kusimamia na kutekeleza majuku yake bila kusukumwa"


Naye Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais -TAMISEMI, Erick Kitale, ameeleza kuwa dirisha hilo la taarifa 'dashboard' linauwezo wakuchukua majira nukta 'code nates' za eneo husika, hali ambayo itakuwezesha kuona hatua za mradi bila udanganyifu badala ya kutumiwa picha za mradi mwingine jambo ambalo lilisambabisha udanganyifu katika hatua za utekelezaji wa miradi ya amendeleo.


Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini (Intergrated Monitoring and Evaluation System)  iMES, umeandaliwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


Awali Mkurugenzi Msaidizi, Divisheni ya Sera na Mipango, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Mwacha, ameyataja malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakurugenzi na maafisa TEHAMA, ili waweza kutumia mfumo huo Jumuishi wa ufuatiliaji wa shughuli zote za serikali kisekta.


Ameeleza kuwa awali kulikuwa na changamoto katika ufuatiliaji wa utekeelezaji wa shughuli za maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kulingana na thamani ya fedha, matumzii ya fedha pamoja na muda wa utekelezaji wa mradi husika.


"Faida za mfumo huu tofauti na mifumo iliyotangulia, mfumo unaonesha mahali mradi ulipo kwa kuzingatia majira nukta zake, idadi ya miradi na gharama zake, matumizi ya fedha, maendeleo ya mradi na hatua zilizoendelea na zilizofikia, miradi ya bakaa na fedha zake" Ameweka wazi Mwacha


Mafunzo ya hayo ya Mfumo wa iMES yametolewa kwa Wakurugenzi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri saba za mkoa wa Arusha, ili kwenda kuwajengea uwezo watumishi wengine katika maeneo yao.







No comments: