WANAWAKE SALE WAMSHUKURU RAIS Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN KWA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 16 November 2023

WANAWAKE SALE WAMSHUKURU RAIS Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN KWA UPANUZI WA KITUO CHA AFYA

 




Na: Elinipa Lupembe - ARUSHA


maipacarusha20@gmail.com


Kata ya Sale iko umbali wa takribani Kilomita 49 kutoka makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro yaliyoko eneo la Waso kata ambayo ina takribani wakazi 6,579, wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji.


Kwa kipindi kirefu hawakuwahi kuwa na kituo cha afya, zaidi walikuwa na zahanati ndogo ya kijiji, ambayo ilitoa huduma ambazo kutokana na ongezeko la idadi ya watu ilifikia kuelemewa na kushindwa kumudu kuwafikia wananchi wote katika utoaji wa huduma  za afya.


Wananchi wa Sale hususani wanawake, walilazimika kwenda eneo la Waso kupata huduma za za kujifungua jambo ambalo liliwagharimu muda na fedha na kusababisha vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua kutokana na ucheleweshwaji wa kupata huduma stahiki.


Aidha, amemshukuru Mama Samia kwa kuwajengea kituo cha afya, kituo ambacho kimewapunguzia mwendo na gharama za kufauata huduma mbali, lakini zaidi kimeondoa vifo vusisvyo vya lazima kwa wanawake na watoto wakati wa kujifungua.


Jenifa Ismael Legina licha ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kujenga kituo cha afya Sale, amethibitisha kituo hicho kutaondoa vifo visivyo vya lazima hasa kwa wanawake wakati wa kujifungua kwa kuwa, kituo hicho kinatoa huduma bora kikiwa na madaktari wazuri wenye moyo wa kuwahudumia 


 "Kuna wajawazito walipoteza maisha kwa kukosa huduma ya kuonhezewa damu, ilikuwa mpaka uenda Waso, kama huna pesa, ilikuwa ni tatizo kwa familia nyingi, wakati mwingine tulilazimika kuchangishana ili mtu akapate huduma, kwa sasa hakuna tena hayo maisha" Ameweka wazi Jenifa.


Jenifa Ismael Legina licha ya kuishukuru serikali kwa kujenga kituo cha afya Sale amethibitisha kituo hicho kutaondoa vifo visivyo vya lazima hasa kwa wanawake wakati wa kujifungua kwa kuwa awali wapo waliopoteza maisha kwa kushindwa kupata huduma kama huduma ya kuongezewa damu.


Bi. Hosiana mama wa watoto watatu ambaye ni mgonjwa wa kwanza kujifunga katoa wodi ya wazazi, amesema kuwa watoto wawili alilazimika kufunga safari mpaka  Waso umbali wa zaidi ya Km 50 kutoka eneo hilo ili kwenda kujifungua jambo ambalo liliwapa gharama kubwa za fedha na muda n lakini wapo kinamama waliopoteza maisha kwa kuchelewa kupata huduma za kujifungua.


"Sisi wanawake wa Sale tunamshukuru Rais wetu, mama Samia ametujali wakinamama, tuna uhakika wa afya za  familia zetu, watoto wawili nilijifungulia Wasao, ukiwa huna pesa unaweza kupoteza maisha" Amesema Hosiana


Awali serikali ilitoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa zahanati na kuwa kituo cha afya na tayari imeshatoa milioni 38.5 kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.

No comments: