Waziri ULEGA AWATAKA WATAALAMU WA MIFUGO NA BINADAMU KUSHIRIKIANA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 16 November 2023

Waziri ULEGA AWATAKA WATAALAMU WA MIFUGO NA BINADAMU KUSHIRIKIANA

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wataalamu katika kongamano la tatu usugu wa vimelea dhidi ya dawa. 


Waziri Abdallah Ulega akizindua muongozo wa matibabu kwa wanyama katika kongamano hilo 


Na Andrea Ngobole, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amewataka wataalamu wa Afya ya binadamu na mifugo kushirikiana kudhibiti ongezeko la usugu wa vimelea na matumizi mabaya ya dawa.


Amesema hayo Leo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kongamano la tatu la kitaifa usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa za binadamu na wanyama.


Amesema asilimia 70 ya magonjwa ya binadamu yanatokana na wanyama hivyo Kuna ulazima wa kujenga ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu wa Afya wa magonjwa ya binadamu na Wanyama ili waweze kupunguza usugu wa vimelea dhidi ya dawa.


Amesema ongezeko la watu Duniani limepelekea kuwa na  mahitaji makubwa ya chakula na dawa na hivyo kupelekea watu kutaka kuchukua dawa bila kuwa na cheti cha daktari na hivyo kupelekea usugu wa dawa kwa magonjwa ya binadamu.


Awali mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela aliwapongeza wataalamu wa Afya kwa kuelimisha uma juu ya madhara ya kutumia dawa bila cheti cha daktari ili kupunguza usugu wa dawa kwa magonjwa ya binadamu.


Amesema kuwa mfumo shirikishi kati ya wataalamu na watendaji wa Serikali ngazi ya Mkoa mpaka kijiji utasaidia sana kupunguza usugu wa dawa.



Mkurugenzi wa mifugo nchini Profesa  Hezron Nonga akizungumza katika kongamano hilo amesema muongozo wa matibabu ya wanyama utawasaidia wataalamu wa Afya za wanyama kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kwa wanyama kabla ya kuwatibu.


Amesema kwa sasa Kuna madaktari wa mifugo 1061, madaktari wasaidizi 4300 na wataalamu wa maabara 70 ambao wamesajiliwa  na  kutambuliwa.

Amesisistiza kuwa kongamano hilo litasaidia kuja na mkakati madhubuti wa kupunguza usugu wa vimelea sugu dhidi ya dawa za binadamu na mifugo

No comments: