AZANIA BANK yaleta faraja Rorya kwa kutoa pikipiki 250 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 21 December 2023

AZANIA BANK yaleta faraja Rorya kwa kutoa pikipiki 250

 




Mwandishi wetu, Maipac Rorya


maipacarusha20@gmail.com


Benki ya Azania Tanzania kupitia Tawi la Lamadi imeibua faraja ya aina yake kwa Wananchi wa Rorya kwa kutoa mkopo wa pikipiki 250 katika kuendeleza programu ya JIKWAMUE KIBIASHARA.


Pikipiki hizo Sasa zinatarajiwa kutumiwa na Makundi ya vijana kujiajiri na hivyo kujiongeza kipato ikiwa ni hatua ya Benki hiyo, kuunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kusaidia vijana kujikwamua na umasikini.


Afisa Mahusiano wa Benji hiyo Tawi la Lamadi Remigius Lilai akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo amesema ni mwendelezo wa kuwasaidia wajasiriamali wadogo kama sera ya nchi inavyoelekeza, kwa nchi nzima


" Tumefikia malengo yetu kwa asilimia 90, kwa kutoa mikopo ya gharama nafuu na marejesho ni nafuu tofauti na mikataba ya watu binafsi", amesema Remigius.


Remigius amesema Ili kuwapata nafasi ya kufanya biashara vizuri wameongeza muda wa marejesho kutoka mwaka mmoja hadi mwaka na nusu,na hiyo inatokana na maombi ya bodaboda.


Amewaomba wanufaika wa mikopo hiyo kuzingatia mikataba waliyoingia sambamba na kufuata sheria za usalama ili vyombo hivyo viweze kutumika vizuri kama ilivyokusudiwa.



Jafari Chege, Mbunge wa Rorya ameishukuru Benki ya Azania kwa kukubali ombi lake la kuwasaidia vijana jimboni kwake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM na kuisaidia serikali kusukuma gurudumu la maendeleo mbele.


Paul Edward Mkazi wa Shirati Rorya ameshukuru Benki hiyo kwa kuwapa mikopo kwa masharti nafuu na kuwa anatarajia kuitumia vizuri Ili imuinue kiuchumi na kuwaomba Azania kuwasogezea huduma mbalimbali ikiwemo za kibenki.


Kwa Mkoa wa Mara benki hiyo ishatoa mikopo ya pikipiki kwa bodaboda wa Wilaya za Bunda, Serengeti na sasa Rorya.


Benki hiyo pia imekuwa Kinara wa kutoa misaada mbalimbali ya kusaidia Jamii nchini.



No comments: