Kamera za Jiji la Arusha zaongeza mapato kutoka sh 2 bilioni hadi sh 6 bilioni - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 22 December 2023

Kamera za Jiji la Arusha zaongeza mapato kutoka sh 2 bilioni hadi sh 6 bilioni

 





Na: Andrea Ngobole, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mpango wa Jiji la Arusha kufunga Kamera katika vituo vyake vyote vya makusanyo ya Kodi na kuweka mfumo wa kielekroniki umeongeza mapato ya Jiji kutoka sh 2 bilioni hadi sh 6 bilioni ndani ya  miezi 10.


Jiji la Arusha limefunga Kamera hizo ikiwa ni mkakati wake wa Kudhibiti kupotea kwa mapato lakini pia kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa watumishi wake.



Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Mhandisi Juma Hamsini alisema anatarajia mapato ya Jiji kuendelea kuongezeka kwani pia vitendo vya rushwa vimeanza Kudhibitiwa.


"Tulinasa tukio la mfanyabiashara mmoja ambaye alikuwa anadaiwa  malimbikizo ya Kodi sh 400 milioni akitaka kumuhonga mfanyakazi wetu milioni 70 wakazungumza hadi ikafika milioni 150"alisema


Hamsini alisema baada ya kunasa tukio hilo na mfanyakazi kugoma kupokea fedha Jiji lilimbana  mfanyabiashara huyo jina linahifadhiwa na Sasa ameanza kulipa deni lake kwa awamu .


"Niwaombe wafanyabiashara kulipa Kodi zao kama ambavyo wanatakiwa njia yoyote ya kukwepa haitawasaidia kwani Sasa Jiji la Arusha linatumia mifumo ya TEHAMA kukusanywa madeni na makusanyo yote na hakuna ambaye anaweza kufuta deni katika mfumo"alisema


Hamsini alisema baada ya kuimarika makusanyo ya fedha Jiji limefunga pia mifumo ya kielekroniki kusajili walipakodi katika ofisini zote za Kata 21 na Kamera zimewekwa.


"Lakini pia tumeongeza posho za wenyeviti wa mitaa kutoka 50,000 kwa mwezi hadi 100,000 ili watusaidie pia kukusanya mapato ya Jiji"alisema


Alisema ongezeko la mapato hayo Sasa limewezesha Jiji kuendelea na miradi mengine ya afya ,elimu na Miundombinu kwa kutumia mapato ya ndani.


Muuguzi mfawidhi wa kituo kipya Cha Afya Mkonoo, Pascal Shingwa alisema wamepokea kiasi cha shilingi 1 bilioni kwa ajili ya ujenzi majengo 9 zikiwepo nyumba za watumishi, jengo la mionzi na maabara Katika kituo hicho cha afya.


Alisema Sasa kituo hicho kinatoa huduma za mama na watoto ambapo wajawazito 20 wanaweza kujifungua kwa siku na kupokea wagonjwa takriban 50 kwa siku.


Khadija Rajabu alisema kabla ya Jiji kuboresha kituo hicho walikuwa wanafata huduma za Afya zaidi ya kilomita 10 Katika hospital ya Kaloleni jijini Arusha.

Shule ya sekondari Terrati


Mwalimu Mkuu shule ya sekondari Arusha Terati, Lilian Manase alipongeza Jiji kwa kutoa zaidi ya sh bilioni mbili kujengwa madarasa 16 katika ghorofa tatu .


"Tuna wanafunzi 966 na tunaendelea na ujenzi wa ghorofa nyingine kupokea wanafunzi wengine zaidi "alisema


No comments: