RC MONGELLA ASISITIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, DAWA, VIFAA NA VIFAA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 30 December 2023

RC MONGELLA ASISITIZA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, DAWA, VIFAA NA VIFAA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza na watendaji kituo cha afya Karatu.



Na Elinipa Lupembe, Karatu


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella ametembelea na kukagua hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma za afya, katika Kituo cha Afya Karatu, na kushuhudia wananchi wakiendelea kupata huduma za afya kama kawaida.


Akiwa kituoni hapo, Mkuu huyo wa mkoa, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Karatu, kusimamia hali ya utunzaji na uhifadhi wa dawa, vifaa na vifaa tiba, huku akisistiza dawa ambazo hazijaanza kutumika, kuhamishiwa kwenye famasi kubwa ya hospitali ya Wilaya, hospitali ambayo inalo eneo maalum la kuhifadhia dawa, badala ya kuziacha kituoni hapo ambapo kuna eneo finyu.


Hata hivyo Mhe. Mongella ameendelea kukerwa na hali ya  utunzaji duni wa vifaa na miundombinu na kuwasisitiza watumishi wa Afya, kuwa wazalendo kwa kuthamini na kuvitunza vifaa vyote,  vinavyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio kuviacha viharibike ovyo.


"Wahudumu wa afya mnalo jukumu la kutunza vifaa na vifaa tiba katika maeneo yenu, ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati mdogo kwa vifaa vinavyohitaji matengenezo madogo madogo badala ya kusubiri viharibike kabisa na kusababisha Serikali kuingia gharama ya kununua upya, jambo ambalo linawezekana kuepukika.


Aidha, amesistiza kuharakisha kutengeneza generata la kituoni ambalo lilipata hitilafu, ili chumba cha kuhifadhia maiti kiendelee kufanya kazi, na kumtaka Mkurugenzi halmashauri ya Karatu kujipanga kukarabati jengo hilo la mochwari.



Hata hivyo, Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Karatu, Dkt. Iman Emmanuel, amesema kuwa,  generata la kituo liliharibika na kupelekwa kwa fundi,  tayari limeshatengenezwa na litarudishwa kituoni hapo kuendelea na kazi, huku akikiri kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa na kujipanga upya kurekebisha changamoto zilizooneka na kuendelea kutekeleza jukumu lao la kuwahudumia wagonjwa na kufikia malengo ya Serikali


Awali, Mhe. Mongella yupo wilayani Karatu kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za  maendeleo kisekta za wilaya hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe John V.K Mongella, amembeba mtoto Mika John (miezi 4), aliyekuwa ameletwa kutibiwa, kwenye Kituo cha Afya Karatu, tarehe 29 Desemba, 2023.

Mhe. Mongella amewapa pole wagonjwa aliowakuta kwenye foleni ya kupata matibabu na kuwahimza kuendelea kutumia vituo vya kutolea huduma za afya, vituo ambavyo Serikali imwekekeza fedha nyinyi za dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja ja wahudumu wa afya.

Awali, Mkuu wa Mkoa huyo, amefanya ziara ya kikazi ya kukagua hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa kwenye kituo hicho cha afya.


No comments: