MTOTO ERICK HONGERA AANZA SHULE NA APOKELEWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 10 January 2024

MTOTO ERICK HONGERA AANZA SHULE NA APOKELEWA

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Mtoto Erick Hongera(6) mkazi wa kata ya Bolo wilayani Malinyi mkoani Morogoro amepokelewa katika shule ya msingi Madibila Juu ambapo ameanza elimu yake ya msingi.


Taarifa za mtoto huyu zilienea kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2023 alipokutwa nje ya jengo la shule wakati watoto wenzake wanaendelea na masomo.


Erick alipoulizwa alisema, anatamani kuwa darasani kama wenzake ila ameshindwa kuanza kutokana na hali duni ya maisha ya kwao. 


Akiongea na Walimu pamoja na Wanafunzi wa shule hiyo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha amesema, Radha alisema amefika shuleni hapo kwa lengo la kuona namna mtoto Erick alivyopokelewa lakini pia na kutoa elimu kwa wanafunzi jinsia ya kujilinda.


Mkaguzi Rasha ameambatana na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Henry Mwangake pamoja na WP Herieth wa Dawati la Jinsia na Watoto kwa lengo la kutoa elimu ya Ukatili kwa Wanafunzi shuleni hapo.


"Tulianza kuona taarifa za mtoto huyu kwenye Vyombo vya Habari na hata alipokuja kuandikishwa haitukushangaza, tumempokea na tutampa ushirikiano kutimiza malengo yake" Amesema  Shida  Lilanga mwalimu Mkuu wa shule hiyo.



Ikumbukwe kuwa Novemba 23, 2023 iliripotiwa taarifa inayomhusu mtoto huyo Erick Hongera ambaye alikuwa na kawaida ya kukaa kando ya majengo ya shule hiyo ya Msingi akiwa mpweke baada ya wazazi wake kushidwa kumudu mahitaji ya kumpeleka shule mtoto huyo.


Kutokana na hali hiyo Askari Polisi kata, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kata hiyo ya Bilo Michael Rasha, limefanikiwa kumsaidia kupitia Jeshi la Polisi na wadau wengine kuwasilisha msaada wa mahitaji ya shule ikiwemo sare za shule, viatu na begi ili kumwezesha kuanza shule mwaka huu.


Mama Mzazi wa Mtoto Erick Consolata Jerimanusi amemshukuru mkaguzi huyo na Jeshi hilo la polisi kwa kufanikisha Mwanae kuanza shule na kutoa wito wenye watoto wenye uhitaji kama huo kutoa taarifa ili waweze kusaidiwa.



No comments: