MVUA ZINAZONYESHA MOROGORO ZASABABISHA VIFO VITATU MMOJA ANUSURIKA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 10 January 2024

MVUA ZINAZONYESHA MOROGORO ZASABABISHA VIFO VITATU MMOJA ANUSURIKA



Athari za Mvua zilizosababisha vufo vya watu watatu mkoani Morogoro








Baadhi ya wananchi mkoani Morogoro wakishuhudia athari za Mvua zilizosababisha vufo vya watu watatu








Na: Lilian Kasenene,Morogoro




maipacarusha20gmail.com




Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia Januari 10,2024, zimesababisha vifo vya watu watatu mkoani Morogoro na mtu mmoja kunusurika kifo, wakati akivuka korongo lililopo karibu na mto Mgolole ambapo maji hayo yalikuwa yakipita kwa kasi.




Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro Shaban Marugujo alisema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari eneo la tukio.




Marugujo alisema vifo vya watu hao vilitokea katika mtaa wa Lukuyu katika kata ya Bigwa manispaa ya Morogoro, huku akiwataja waliofariki kuwa ni kuwa niTheresia Adolf(73), Mwanahamis Issa(35) na Asnath Thomas(6) ambapo aliyenusurika kifo akiwa Sengo Hamis(47) ambaye alisema alipanda juu ya mti kwa zaidi ya saa nne.




“Tulipata taarifa za tukio hili majira ya sa mbili asubuhi ya leo lakini tukio limetokea kati ya saa saba usiku,hapo tunaona namna muda ulivyopotea bila taarifa kutolewa, lakini taarifa ingetolewa mapema uwezekano wa kuwaokoa waliofariki ingewezekana,”alisema.




kamanda huyo alisema miili miwili pekee ndio imeopolewa kati ya mitatu, afuta na juhudi za kut mwili mmoja zinaendelea ambaye ni Mwanahamis.




Aidha aliwataka wananchi kuacha tabia ya kupima majikwa kuona ama kuweka mti huku akiwataka kuhakikisha kusubiri maji kupungua ama kuchuku tahadhari nyingine zaidi.




Akizugumza tukio hili mwenyekiti wa mtaa wa Bigwa standi Benjamin Suzee alisema Sengo alipoona maji hayo alitoa taarifa za yeye na familia yake kusombwa na maji baada ya yeye kujiokoa na kupanda juu ya mti ambapo aliwataka wananchi wa mtaa wake kuhakikisha wanachukua tahadhari wakati wotw hasa kipindi hiki cha mvua ambapo pamekuwa na matukio mbalimbali ya watu kusombwa na maji ama kuingiliwa na maji.




Familia moja katika kata hiyo ya Bigwa ndio imepoteza Bibi, mama na mtoto mdogo, na majeruhi wa mafuriko hayo amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro.




Mwisho.

No comments: