PORI LA AKIBA WAMI MBIKI LATAKIWA KUJITANGAZA ZAIDI. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 12 January 2024

PORI LA AKIBA WAMI MBIKI LATAKIWA KUJITANGAZA ZAIDI.

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro

maipacarusha20@gmail.com


Kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii imeagiza mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania(TAWA) kufanya jitihada  za kutangaza utalii katika pori la akiba la wami mbiki pamoja na  kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuleta tija katika sekta ya utalii hapa nchini.


Maagizo hayo yametolewa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Thimotheo Mnzava wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya  kukagua na kutembelea miradi  inayotekelezwa na TAWA.


Aidha kamati hiyo imejionea ujenzi wa geti la kupokelea wanyama pori  waliotekelezwa na familia zao na maeneo maalumu ya kuwatunza wanyama hao .


Mnzava amesema kuwa mradi huo ni muhimu na utasaidia kuongea watalii katika pori hilo la AKIBA na mapato serikalini, hivyo ni lazima kuwepo na miundombinu wezeshi itakayowavutia watalii.


Hata hivyo amepongeza utekelezaji wa mradi huo na kwamba unaendana na kukidhi vigezo ikilinganishwa na fedha iliyotolewa.


kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dustan Kitandula amesema mikakati iliyopo ni  kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu ya kuhifadhi wanyama na kuongeza idadi kubwa ya watalii katika pori hilo, ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato.


Hata amebainisha kuwa huduma inayotarajiwa kutolewa Katika pori hilo la akiba la Wami Mbiki itakuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii.


"Kila mmoja atatamani kuja kwaona wanyama waliotelekezwa na familia zao tangu walipopokelewa hadi walivyo kwa kipindi hicho," amesema Naibu Waziri Kitandula.



Aidha Kitandula amesema kuwa pori la akiba la Wami Mbiki linatarajia kupokea watalii zaidi ya 50 kila mwezi mara tu mradi huo utapokamilika.






No comments: