Wanachama wa KAGERA UMOJA ASSOCIATION (KUA) Wakicheza nyimbo za asili ya Mkoa wa KAGERA. |
Wanachama wakiburudika Kwa nyimbo za asili |
Mwenyekiti wa KAGERA UMOJA ASSOCIATION Gosbert Shausi akizungumza na wanachama katika sherehe za kuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
Kikundi Cha Kagera Umoja Association(KUA) kilichopo mkoani Morogoro katika sherehe kuaga Mwaka 2023 na kukaribisha Mwaka mpya wa 2024, kimewataka wanaumoja huo kuendelea kushirikiana, pamoja na kukumbukana kwenye Raha na shida.
Akizungumza wakati sherehe hiyo mwenyekiti wa Gosbert Shausi alisema wanaumoja huo wamekuwa wakifanya sherehe hizo kila Mwaka na wamekuwa wakijumuika na familia zao.
Shausi alisema pamoja na kukutana kwao kila Mwezi na kuzumgumza mambo wamefanikiwa kuwa na uwanja ambapo wameanza ujenzi na ndipo patakuwa sehemu ya kukutania wanaumoja hao.
Alisema sherehe yao ya mwaka huu imekuwa na utofauti ambapo wameacha kufanyia kwenye kumbi za ndani na Sasa kutoka nje ya mji ikiwa ni pamoja na kuangalia vivutio vilivyopo kwenye milima ya uluguru.
"Tumefanya huku nje ya mji ili wanachama waone vivutio na kuangalia mandhari nyingine na sasa tumekuja huku," alisema Mwenyekiti huyo.
Mmoja wa wanaumoja huo wa KUA Loveness Nyawili alisema kukutana kwao kunawajenga kuendeleza upendo pamoja na kushikamana zaidi katika Kila hari.
Katika sherehe hiyo nyimbo mbalimbali za kabila la wahaya kutoka mkoani Kagera zilipigwa na wanaumoja kuzicheza kwa furaha.
No comments:
Post a Comment