WAZIRI MCHENGERWA AAGIZA AFISA ELIMU WA HALMASHAURI NA MIKOA KUSAJILI SHULE ZILIZOKAMILIKA KWA ASILIMIA 70 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 8 January 2024

WAZIRI MCHENGERWA AAGIZA AFISA ELIMU WA HALMASHAURI NA MIKOA KUSAJILI SHULE ZILIZOKAMILIKA KWA ASILIMIA 70

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa






Na: Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa ametoa agizo kwa maafisa elimu nchini kuhakikisha wanasajili shule zote mpya zilizokamilisha ujenzi na ambazo zimefikia asilimia zaidi ya 70 ya ujenzi wake ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024.

Mchengerwa ametoa agizo hilo wakati akifunga kikao kazi cha Makatibu Tawala wasaidizi na Maafisa Elimu wa Halmashauri kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa kutokana na Hali ilivyo ya uhitaji wa shule Katika kipindi hiki hakuna haja ya kusubiri shule ikamilike kwa asilimia 100 ndo isajiliwe itakuwa ni ucheleweshwaji asio na sababu za msingi.

"Kama shule ni mpya na imejengwa na kuifikia asilimia 100 ya ujenzi wake haina haja ya kusubiri, isajiliwe hivyohivyo ili Wanafunzi waanze kuingia na kuanza kusoma hii itasaidia watoto wote waliofaulu kujiunga na kidato Cha kwanza kwenda shule kama ilivokusudiwa" alisema waziri mchengerwa.

Aidha alisema kuwa shule hizo ambazo zimekamilika kwa asilimia 75 zinapaswa kusajiliwa kwa wakati ikiwa ni pamoja kuhakikisha maeneo yote yanapatiwa hati miliki Kwa ajili ya matumizi ya shule.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima alisema kuwa Katika kuendelea juhudi za elimu mkoa umewekeza zaidi billion 37 Kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya shule.

Aidha pia alisema fedha hizo zitatumika kujenga shule ya bweni ya wasichana Ili kumlinda mtoto wa kike na aweze kupata elimu na kutimiza ndoto zake Katika maisha.

Malima pia aliwasisitiza walimu kuanza kutengeneza kizazi chenye uzalendo kuanzia shule ya awali watoto wanapoanza kuingia shuleni Ili tuweze kuwa na taifa lenye uzalendo Katika sekta zote.

Naye kaimu katibu mkuu Dk Charles Msonde alisema kuwa Katika kuwajibika na uadilifu wa kuboresha elimu ya msingi na secondari ni lazima kuwe na mapinduzi makubwa kuanzia elimu ya awali.

Hata hivyo alibainisha kuwa maboresho Katika lugha ni muhimu sana Katika kuinua elimu ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha walimu wanapata huduma stahiki , kulindwa pamoja na kuondoa chamoto mbalimbali zinazowakabili.


No comments: