DIWANI AWEZESHA MAFUNZO JUKWAA LA WANAWAKE PANZUO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 21 February 2024

DIWANI AWEZESHA MAFUNZO JUKWAA LA WANAWAKE PANZUO

 





Na: Mwandishi wetu, Maipac MKURANGA 


maipacarusha20@gmail.com


DIWANI wa Panzuo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Dude Hamis amewezeaha mafunzo ya ujasiriamali kwa Jukwaa la Wanawake  wa kata hiyo.

Jukwaa hilo limepatiwa mafunzo na wakufunzi kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii, kilimo, Mifugo na Ustawi wa Jamii wa Kata hiyo .

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo uliofanyika katika kata ya Panzuo Dude alisema lengo ni kuhakikisha Jukwaa hilo linafanya shughuli zake kwa kufuata taratibu hususani upande wa ujasiriamali.

Amesema wananchi wanapokuwa na shughuli zao za kufanya wakiwa na elimu ya kuziendesha inasaidia kuondoa manung'uniko kwa viongozi wakiwalaumu kila mara.

"Wakishapata mafunzo hapa wataenda kufanya shughuli zao kwa kufuata kanuni na taratibu na kila mtu sasa atasimamia kwenye eneo lake na kupata tija kwa anachokufanya hapa itapunguza kupata muda wa kusimama kwenye malalamiko" amesema.

Amesema mbali ya mafunzo hayo amekwisha kuwakutanisha vijana kwenyw michezo, pia upande wa elimu amewezlzesha uandaaji wa mashamba kwenye shule zote kwa ajili ya kulima mazao ya chakula Cha wanafunzi shuleni.

Ameahidi kuendelea kufadhili mafunzo hayo mara kwa mara Ili vikundi vya wanawake vinapokopa view na biashara endelevu na kurejesha mikopo kwa wakati

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Fatuma Challa amemshukuru Diwani huyo kwa hatua hiyo huku akieleza kwamba kilimo na biashara watakazofanya sasa zitakuwa na tija kutokana na elimu waliyopata.

Zakia Msangi  kutoka Kijiji Cha Nyatanga amesema awali waliokuwa wakifabya kilimo na ufugaji bila kufuata taratibu lakini sasa wanakwenda kuwa na mabadiliko makubwa kwenye maeneo hayo na kuinuka kiuchumi.



No comments: