Maandamano ya Chadema Arusha yaleta msisimko - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 28 February 2024

Maandamano ya Chadema Arusha yaleta msisimko



Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na Viongozi wengine wa chama hicho wakiongoza maandamano huku mvua kubwa ikinyesha jijini Arusha




Na Mwandishi Wetu, Arusha

maipacarusha20@gmail.com

Maelfu ya watu wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani wamejitokeza katika maandamano yaliyoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha picha ya mvua kunyesha Kwa zaidi ya masaa mawili.



Maandamano hayo yaliyoanzia asubuhi katika vituo vya TANAPA, Morombo, na Kwa Mrefu na kufikia kilele chake katika viwanja vya reli vya Unga Limited jijini Arusha.

Waandamanaji hao, waliotembea umbali wa zaidi ya kilomita 30, hawakurudi nyuma hata baada ya kunyesha kwa mvua kubwa. Wakiimba nyimbo za hamasa kubwa wakitaka katiba mpya.




 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe,ndiye aliongoza maandamano hayo, na kusisitiza Katiba mpya na haki kwa wananchi.

Mbowe akizungumza katika mkutano huo,alilaani matumizi mabaya ya kodi za umma na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka.


Viongozi wengine walioshiriki maandamano hayo ni pamoja Makamu Mwenyekiti Bara, Antipas Lisu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, walisisitiza umuhimu wa serikali kusikiliza kilio cha wananchi na kuchukua hatua za haraka.




Maandamano haya yalivutia watu kutoka maeneo mbalimbali ya Arusha na hata mikoa jirani.


Wananchi wameahidi kuendelea kupaza sauti zao hadi haki itakapopatikana na maisha bora kwa kila Mtanzania yatakapohakikishwa.




"Licha ya kutembea kilomita zaidi ya 30 huku mvua zikinyesha takriban masaa mawili bado watu hawakukubali kusitisha maandamano taswira hii inaashiria Watanzania wanataka mabadiliko na sio kudanganywa kwa siasa za uongo," Amesema Mbowe.


Amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kufuja kodi za wananchi kusafiri kwenda nje makundi ya watu suala ambalo ni ubadhilifu wa mali za umma
na kuwaumiza walipa kodi wanaoishi maisha duni.




Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Lissu amesema Watanzania wamechoka kwa kutosikilizwa na serikali iliyopo madarakani hivyo maandamano yataendelea mpaka haki ipatikane.





Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Lema ameitaka serikali ya Mkoa wa Arusha kuachana na vikwazo na sababu zisizo za msingi pindi maandamano yanapoitishwa, kwani maandamano ni ishara inayoashiria wananchi kuionyesha serikali kuwa wamechoka na wanataka haki.




"Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu naamini serikali itafanyia kazi kwa hiki kilichofanyika leo" amesema Lema.


Kwa upande wake, wakili, Boniface Mwabukusi amesema maandamano hayo ni hatua kamili ya kupata kinachotakiwa na Watanzania wote.

"Nawapongeza sana kujitokeza na kuvumilia licha ya mvua kubwa zilizonyesha lakini bado mliendelea kwa sababu mnachokitaka ni maisha Bora na upatikanaji wa huduma za Jamii ambazo bado hazipatikani kutokana na Chama Cha Mapinduzi kilichoko madarakani lwa zaidi ya miongo sita sasa, ".amesema Mwabukusi na kuongeza.

Katika maandamano hayo pia alishiriki Dk Wilbroad Slaa ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu Chadema Viongozi wengine wa Chadema Joseph Mbilinyi, John Heche na wengine kadhaa 


No comments: