PROFESA KABUDI AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHENYE MIAKA 58 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 28 February 2024

PROFESA KABUDI AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHENYE MIAKA 58

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Mbunge wa jimbo la Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhi gari la kubeba wagonjwa wa dharula (Ambulance) katika kituo cha afya Magubike wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro yenye thamani ya shilingi milioni 170.


Kukabidhiwa kwa gari hilo ni jitihada za serikali katika kuboresha utoaji wa huduma katika kituo hicho cha afya.


Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo kituoni hapo Profesa Kabudi amemshukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari hiyo kwani itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.


Aidha Prof Kabudi amewataka wananchi na watumishi kuitunza gari hiyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika uboreshaji wa huduma za afya nchini.


Naye mganga mkuu wa wilaya ya Kilosa Dk Mameritha Basike amesema ujio wa gari hiyo itasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vilikuwa vikitokea sababu ikiwa ni kukosa gari la kubeba wagonjwa mahututi na hata kutaka kuokoa maisha ya mama wajawazito wanapopata tatizo.


Mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Magubike Dk Asha Hembela akiishukuru serikali kwa hatua hiyo ambayo itasaidia kuondoa changamoto za usafirishaji wagonjwa wa dharula kituoni hapo.


Diwani wa kata ya Magubike Abuu Msophe amebainisha mafanikio makubwa walioyapata katika sekta ya afya huku wananchi wa kata hiyo wakionyesha kufurahishwa na ujio wa gari hiyo kwani itakuwa mkombozi kwao.


Kituo hicho chenye miaka 58 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1966 kinacho hudumia takribani kata sita awali kilikuwa kikitumia gari ndogo katika kutoa huduma hiyo jambo ambalo lilikuwa halikidhi mahitaji katika kuhudumia wananchi hasa huduma ya mama na mtoto.




No comments: