SUA, USAID,TAOTIC YAANZISHA MASHINDANO KUSAKA VIJANA WABUNIFU KATIKA KUBORESHA KILIMO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 20 February 2024

SUA, USAID,TAOTIC YAANZISHA MASHINDANO KUSAKA VIJANA WABUNIFU KATIKA KUBORESHA KILIMO

 

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima






Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa ushirikiana na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), taasisi ya vitovu vya ubunifu(TAOTIC) pamoja na Idara ya Kilimo ya Marekani(USDA) wameanzisha mashindano ya kusaka vijana wabunifu watakao tengeneza program za kusaidia wakulima kuboresha kilimo nchini, kwa kutumia teknolojia rahisi za kilimo .


Mkurugenzi  msaidizi wa sayansi na teknolojia kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Alexandaer Mtawa amesema hayo mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo yanayoendeshwa kupitia mradi wa YEESI LAB yanayohusisha vijana wabunifu kwenye masuala ya kilimo.


Amesema Mashindandano hayo yamelenga kuwaandaa  vijana watakaokuwa tayari kushiriki  kubuni teknolojia rahisi itakayowasaidia wakulima wadogo hususani walioko vijijini.


Aidha Mtawa amesema kuwa pamoja na kuwaandaa vijana kubuni teknolojia katika kilimo pia wanatakiwa kuanzisha makampuni mbalimbali yatakayowasidia katika suala zima la utekelezaji wa shughuli zao za kila siku hususani katika kilimo.


Mkuu wa mradi huo kutoka SUA Dk Kadeghe Fue amesema kuwa vijana wote watakaoshiriki shindano hilo na kufanikiwa watanufaika zaidi na masuala ya teknolojia na ubunifu katika kilimo ikiwa ni pamoja na kujipatia kipato chenye tija katika familia na taifa kwa ujumla.


Hata hivyo ameendelea kueleza kuwa manufaa watakayopata vijana katika mradi huo wa YEESI LAB. yatakuwa na mafanikio ya wakulima wote na watanazania kwa ujumla, hivyo basi vijana hao ni muhimu sana na watakiwa kushikwa mkono ili kuendeleza bunifu zao kwa wakulima.


Aidha amesema kuwa lengo kubwa la mradi huu ni kuhakikisha wakulima wanafaidika  na bunifu hizo hususani wale walioko vijijini ili wawze kujikwamua kiuchumi .


Mkuu wa mkoa wa Morogoro  Adam Malima amewataka vijana wanaoshiriki shindano hilo  kuwa na ushirikiano na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yao  ili waweze kukubalika katika jamii .


Hata hivyo mkuu huyo ameaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vijana hao ambao utakuwa ni muhimili mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ndani na nje ya mkoa wa Morogoro.


Mkuu wa mkoa pia amewataka vijana hao kuzingatia umuhimu kuweka a kipaumbele  katika  mazao ya kimkakati ikiwemo zao la karafuu.



No comments: