Breaking News; Aliyefungwa miaka 23 kwa Ujangili atoroka Magereza,Msako mkali umeanza - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 23 March 2024

Breaking News; Aliyefungwa miaka 23 kwa Ujangili atoroka Magereza,Msako mkali umeanza

 

Amos Bernard Mtinange maarufu Kwa jina la Meja asiku alipokamatwa na twiga



Mwandishi wetu, Babati


 maipacarusha20@gmail.com


Mfungwa Amos Bernard Mtinange maarufu kama Meja  aliyekuwa anatumikia kifungo cha 23 kwa tuhuma za Ujangili ametoroka akiwa chini ya Ulinzi, wilayani Babati mkoani Manyara.


Mfungwa huyo ametoroka akiwa katika shamba la magereza na alihukumiwa kifungo hicho mwezi Novemba mwaka Jana.


Mkuu wa magereza mkoa wa Manyara(RPO),Solomon Mwambingu amethitisha Jana kuwepo taarifa za  kutoroka kwa mfungwa huyo.


"Tunazohizo taarifa na suala hili linafanyiwa kazi "amesema Mkuu huyo wa Magereza 


Hata hivyo , Mkuu huyo Magereza hakuwa tayari kuelezea mazingira ya kutoroka mfungwa huyo na hatua ambazo tayari zimechukuliwa.


Meja anadaiwa kutoroka wiki iliyopita akiwa na mfungwa mwingine ambaye hata hivyo mfungwa huyo amekamtwa.


Uchunguzi wa tukio hili la aina yake bado unaendelea na taarifa zaidi zitatolewa.


Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi wanyamapori (TAWA) na Askari wa Burunge WMA na chemchem walieleza kushangazwa na kutoroka kwa mfungwa huyo.


"Tunaimani kubwa la Jeshi la Magereza na vyombo vingine vya Ulinzi kuwa mfungwa huyu atakamatwa kwani mazingira ya kutoroka yanautata mkubwa"alisema Afisa mmoja wa TAWA.


Askari mwingine ambaye alikuwa katika kikosi kilichoshiriki kumkamata Meja alisema ,haikuwa rahisi kukamatwa kwani kwa zaidi ya mwaka mmoja aliwekewa mitego lakini alikwepa.


"Hizi taarifa zimenishangaza sana ,tuliambiwa alitoroka akiwa na mwenzake mmoja ambaye tayari amekamatwa ....kwa kazi kubwa tuliyofanya kumkamata lakini pia polisi,Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mahakama kwa kulisimamamia suala hili tunaimani kubwa juhudi hizi hazitapotea bure"alisema Julius Peter 


    Meja  alipofungwa miaka 23



Mahakama ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa wilaya ya Babati mkoa Manyara, ilimuhukumu kwenda jela miaka 23  , Amos Benard  Mtinange maarufu kwa jina la Meja baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili ya  uhujumu uchumi ya ujangili wa Twiga na kuuza nyama za Twiga kinyume cha sheria.


Meja alikamatwa  April 20 mwaka 2023  saa kumi na moja jioni  maeneo ya mfulwang'ombe kwenye Kambi ya samaki Kijiji cha Vilima vitatu, ndani ya eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge wilayani Babati ,mkoa wa Manyara baada ya kusakwa muda mrefu kutokana na kujihusisha na ujangili wa Twiga na kufanya biashara ya nyama za Twiga. 


 Alikamatwa kutokana na mtego  ulioandaliwa na askari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA),Jeshi la polisi, Askari wa Burunge WMA na askari wa Taasisi ya Chem chem association ambayo imewekeza shughuli za Utalii katika eneo hilo na kugharamia vikosi vya Kupambana na ujangili.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Babati, mkoa wa Manyara, Victor Kimario alisema,  mahakama imemtia hatiani  Meja baada ya kujiridhishwa pasi na shaka kuwa amekuwa akijihusisha na ujangili wa Twiga na kuuza nyama za Twiga.



Alisema ili kukomesha matukio ya ujangili nchini, Mahakama inamuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 23 jela. 


Kabla ya hukumu hiyo, Meja aliomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anafamilia ambayo inamtegemea.



Hata hivyo, Waendesha Mashitaka Mawakili wa Serikali   Benedict Mapunda,na Mawakili wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori(TAWA) Getrude Kariongi na  Shahidu Kajwagya,walipinga kupunguziwa adhabu mtuhumiwa huyo.


Wakili Kariongi alisema kesi  inayomkabili mtuhumiwa huyo ni ya uhujumu uchumi na ambacho amekuwa akifanya muda mrefu ni kuuwa Twiga ambao ni kivutio cha Utalii nchini lakini pia mnyama huyo anachangia pato la taifa.



Alisema wanyamapori huchangia kupatikana fedha za kigeni ambazo ndizi zinachangia  kupatikana fedha za miradi ya serikali ikiwepo ujenzi wa shule, kuchangia gharama za afya na nyingine.



Katika kesi hiyo, Jamuhuri ilikuwa na mashahidi saba ambao  ambao walikuwa ni mtunza vielelezo vya polisi,Askari wawili walioshiriki kumkamata , Mtambuzi na mtathimini wa nyara za serikali,Mtaalamu kutoka Forensic .Mpelelezi wa kesina Mlinzi wa Amani ambaye alikuwa ni hakimu.


No comments: