TFS YASEMA MISITU KUTUMIKA KATIKA UBUNIFU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 21 March 2024

TFS YASEMA MISITU KUTUMIKA KATIKA UBUNIFU

 


Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Kamishana wa Uhifadhi,Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema umefika wakati wa Misitu kutumika katika Ubunifu ili kutatua changamoto mbalimbali za kidunia na kuifanya dunia kuwa sehemu salama.


Amesema hayo Wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye taasisi za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari na kwenye makazi, katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani na siku ya upandaji miti kitaifa yanayoadhimishwa katika Wilaya humo, kauli mbiu ikiwa Misitu ni Ubunifu.


Prof Silayo amesema ubunifu huo unazingatia kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo masuala ya Sera zinazosimamia rasilimali Misitu, Teknolojia pamoja na uchumi.


"Upandaji wa miti lazima uwe na usimamizi, shirikishi na kuimarisha Uhifadhi wa Maliasili,lakini tukumbuke kuwa sisi tunahitaji zaidi Misitu kuliko Misitu inavyotuhitaji,"amesema.


Balozi wa mazingira Tanzania Ahidi Sinene ametoa rai kwa watanzania kuendelea kupanda miti mashukeni kwa wingi hasa ya matunda ili kuondoa udumavu.


"Mtu anayehatibu Mazingira ni mtenda dhambi kama walivyo watenda dhambi wengine, na tangu nimekuwa balozi nimeweza kupanda miti 10,000 peke yangu na naendelea kuhamasisha kwa kujitokeza,"amesema.


Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Same Elizabeth Mkongo ameshukuru TFS kwa kupitia shule hiyo miti 260, huku akiiomba kuwaongezea miti mwingine hasa ya matunda.


Shule ya msingi Same ina zaidi ya wanafunzi 860 na imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha wanafunzi kupanda miti kuanzia shuleni Hadi majumbani kwao.


Kilele Cha maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani na siku ya upandaji miti kitaifa inatarajia kuwa Machi 21,2024 na kitaifa yatafanyika wilayani Same mkoani Kilimanjaro ambapo makamu wa Rais Dk Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.


No comments: