Wadau wa Kilimo na ufugaji IKOLOJIA wakizungumza na MAIPAC Media Tanzania |
Mratibu warsha hiyo, Erimelinda Temba akizungumza na wadau wa kilimo |
Na: Mussa Juma, maipac
maipacarusha20@gmail.com
Wakulima na wafugaji nchini, wameshauriwa kutumia mbinu za asili katika Kilimo na Ufugaji (Kilimo Ikolojia) ili kupunguza matumizi makubwa ya dawa za viwandani.
Kilimo na Ufugaji wa asili pia mazao yake yana bei za juu katika Soko la Dunia na ni Salama zaidi kwa afya za walaji na wakulima.
Mkurugenzi wa Taasisi ya ECHO EAfrika Erwin Kinsey alitoa ushauri huo,katika warsha ya wadau wa Kilimo Ikolojia mkoa Arusha ambayo iliwashirikisha wakulima, wafugaji na wanafunzi wa vyuo vya Kilimo na Watendaji wa Serikali ambayo ilifanyika jijini Arusha.
Kinsey alisema, wakulima na wafugaji wanaujuzi wa asili ambao ni bora zaidi kuliko Kilimo cha kisasa ambacho kina matumizi makubwa ya kemikali kuanzia kulima, kupanda, kuvuna na kuhifadhi mazao.
"Tuendeleze Kilimo Ikolojia kwani pia ni Salama zaidi kwa Afya ya mkulima na mlaji mfano wagogo wana mbinu nzuri za kutunza mazao Yao bila dawa tujifunze "alisema
Mratibu warsha hiyo, Erimelinda Temba alisema warsha hiyo hufanyika Kila mwaka ili kuendelea uzalishaji wa Kilimo lkolojia ili kuwa na uzalishaji endelevu wa chakula.
Temba alisema kuna umuhimu wa kuwa na Ufugaji na Kilimo Ikolojia ili kuboresha uchumi wa Jamii kwa ujumla kwa gharama nafuu zaidi.
"Unatumia mbolea ya mifugo katika Kilimo, unatumia dawa za asili Katibu Mifugo lakini pia unatumia wadudu waliopo ardhini kuboresha Afya ya ardhi na wengine kusaidia kutibu magonjwa "alisema
Mwenyekiti wa vikundi vya Maendeleo vya wakulima na wafugaji Longido, Nambori Nabaki alisema Kilimo Ikolojia kimekuwa na manufaa kwao kwani wanapunguza gharama za mbolea za viwandani na dawa za Mifugo.
Hata hivyo aliomba wafugaji kusaidiwa kupata tiba ya ugonjwa wa mbuzi na Kondoo wa Olmiro ambao umeanza kuuza Mifugo Yao
Akizungumzia ugonjwa huo Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Arusha DC, Linus Prosper alisema ugonjwa huo unasambazwa na mbwa na kuwataka wafugaji kuchanja mbwa wao.
"Ugonjwa huu unatokana na minyoo ya mbwa na husambazwa kupitia kinyesi chake na mbuzi na Kondoo wakila nyasi zenye kinyesi wadudu huingia hadi kichwani na kumfanya mbuzi au Kondoo awe na kizunguzungu na asipopata tiba ambayo hufa"alisema
Mwenyekiti wa vikundi vya Maendeleo vya wakulima na wafugaji Longido, Nambori Nabaki akizungumza na waandishi wa Habari nje ya warsha hiyo |
No comments:
Post a Comment