TAWIRI YAPOKEA VIFAA VYA UTAFITI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 240 KUTOKA USAID - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 5 March 2024

TAWIRI YAPOKEA VIFAA VYA UTAFITI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 240 KUTOKA USAID







Na Mwandishi Wetu, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Taasisi ya Utafiti wa  Wanyamapori Tanzania  (TAWIRI) imepokea vifaa vyenye thamani yaTsh. 242,000,000 kutoka Shirika  la Maendeleo la Kimataifa la Marekani USAID kupitia  mradi wake wa Tuhifadhi  Maliasili.


Akizungumza katika hafla ya  makabidhiano iliyofanyikia Makao makuu ya TAWIRI, Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya TAWIRI Dkt. David Manyanza ameishukuru USAID kutoa vifaa ambavyo ni muhimu  katika tafiti za wanyamapori  hususan sensa ya wanyamapori ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili hadi mitatu.


"Kama alivyowahi kusema Hayati Rais. Ali Hassan  Mwinyi, mali bila daftari  hupotea bila habari hivyo  hatuna budi kuidadi wanyamapori ili kuwa na uhifadhi endelevu wa wanyamapori hapa chini "ameeleza Dkt. Manyanza.


Dkt. Manyanza amesema vifaa hivyo vina mchango mkubwa kwenye sekta ya Maliasili kwani tafiti za TAWIRI zinasaidia kuzishauri  mamlaka za uhifadhi, "nitoe   wito kwa wadau kujitokeza kushirikiana na TAWIRI ili kuwezesha tafiti za wanyamapori kwa ustawi wa  uhifadhi na  kukuza utalii " ameeleza Dkt. Manyanza.

 


Kiongozi wa Idara ya mazingira na usimamizi wa Maliasili kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), Nathan Sage, amesema kwa miaka 60 sasa, USAID imekuwa ikishirikiana Tanzania kuhifadhi bioanuwai  ikizingatiwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali  za kibaolojia ikiwemo maliasili ya Wanyamapori  ambao wana thamani kubwa ya kitamaduni, kiuchumi na  kielimu.


Aidha, Bw. Sage amesema  katika kuendeleza ushirikiano huo, USAID  imetoa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 242 kwa TAWIRI ili kuimarisha uhifadhi kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia kurahisisha tafiti za wanyamapori


Kwa upande  wake  Mkurugenzi Mkuu TAWIRI  Dkt. Eblate Mjingo amesema Jukumu kuu la TAWIRI ni kufanya tafiti za wanyamapori ambapo ameishukuru USAID kutoa vifaa ambavyo ni Kamera za kufunga kwenye ndege wakati wa kuidadi wanyamapori, Mikanda ya visukuma mawimbi ya Tembo (GPS Collars) na Vifaa vya Majira  nukta (_Location GPS_)

 "Utafiti ni gharama, unahitaji  vifaa  na teknolojia, hivyo vifaa hivi tulivyopokea vinakwenda kusaidia sana hususani kwenye sensa ya wanyamapori.

No comments: