Na: Mwandishi wetu,Dar es Salaam
maipacarusha20@gmail.com
Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF) kupitia Programu ya Ruzuku Ndogo inayotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limesaini makubaliano ya kutoa sh 4.04 bilioni kwa mashirika yasiyo ya kiserikali 44 nchini ili kutekeleza miradi ya Uhifadhi wa Mazingira, Misitu, kuendeleza ufugaji nyuki, kutunza vyanzo vya Maji na uwezeshaji Jamii kiuchumi.
Utiaji saini wa Makubaliano hayo umefanyika leo April 4, 2024, katika Makao Makuu ya Jengo la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na kuongozwa na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP ndugu Shigeki Komatsubara.
Miongoni mwa mashirika yaliyosaini mkataba kupatiwa fedha hizo ni shirika la Wanahabari wa jamii za pembezoni(MAIPAC) ambalo limekuwa likitekeleza miradi ya uhifadhi wa mazingira, Misitu na vyanzo vya maji na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa maarifa ya asili.
Akizungumza katika hafla hiyo, Komatsubara amesema kuwa mashirika zaidi ya 400 yalituma maombi kuomba fedha za kutekeleza miradi midogo midogo nchini Tanzania bara na Zanzibar lakini ni mashirika 44 tu ndio yamefanikiwa.
"Hongereni sana leo kuwa miongoni mwa mashirika na asasi ambazo zimepata fursa kutekeleza miradi midogo Tanzania.
Komatsubara amesema anaimani kubwa mashirika ambayo yanapewa fedha hizo yatakwenda kutekeleza vyema miradi ambayo itagusa jamii hasa wanawake, vijana, walemavu na jamii za pembezoni.
"Tunatarajia miradi yetu itakwenda kuchochea maendeleo katika jamii ikiwepo pia kukabiliana na vichocheo vya uharibifu wa mazingira" amesema
Naye Mwakilishi kwa niaba ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Lilian Lukambuzi akizungumza katika hafla hiyo alitaka mashirika yaliyopewa fedha hizo kuzitumia kama ilivyokusudia.
Amesema serikali itafuatilia miradi ambayo inakwenda kutekelezwa ili kuhakikisha inakuwa na tija.
Awali Mratibu wa Programu ya Ruzuku Ndogo za GEF nchini, ndugu Faustine Ninga amesema haikuwa kazi rahisi kupitisha mashirika hayo machache kupata ruzuku kutokana na uhitaji mkubwa kutoka katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema kamati ya Uendeshaji ya programu hiyo ya Ruzuku Ndogo za GEF ambayo inaundwa na wataalam kutoka sekta mbalimbali na taasis zisizo za Kiserikali kwa kushirikia na UNDP ilifanya kazi kubwa ya kuchambua maandiko ya miradi zaidi ya 400.
Hata hivyo,amesema kutokana na uhitaji kuwa mkubwa ni mashirika 44 tu ndio yalipitishwa, ijapokuwa mashirika mengine yalikuwa na madokezo mazuri ya miradi.
Hata hivyo ameyataka mashirika haya kufuata kanuni na taratibu za nchi na miongozi ya uendeshaji wa taasisi zisizo za kiserikali katika utekelezaji wa miradi yao ili miradi iwe na matokeo mazuri.
Amesema kamati ya ufuatiliaji miradi hiyo itakagua na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ili kuhakikisha kuwa jamii zinanufaika .
Wakizungumza baada ya kusaini mikataba baadhi ya watendaji wa mashirika hayo walipongeza UNDP kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi midogo katika jamii.
Mwakilishi mkaazi wa UNDP Shegeki Kamatsubara akimpongeza mkurugenzi wa MAIPAC Mussa Juma baada ya kisaini mkataba wa kupewa ruzuku |
Mkurugenzi wa shirika la MAIPAC Mussa Juma alisema hii ni mara ya pili shirika hilo kupata fedha na kueleza katika miradi iliyopita kulikuwa na matokeo mazuri.
"Tulikusanya maarifa ya asili katika uhifadhi mazingira, misitu na vyanzo vya maji na kufanikiwa kutengeneza kitabu cha kwanza nchini cha umuhimu wa maarifa ya asili ambacho kilizinduliwa na Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Seleman Jafo na kugawanywa bure katika shule,taasisi za serikali na binafsi"alisema
Alisema pia waliweza kushirikisha watungaji wa sera kutambua umuhimu wa kulinda na kuendeleza maarifa ya asili ikiwepo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
"Safari hii maarifa ya asili yatakusanywa na kuhifadhiwa katoka vitabu na katika vyombo vya habari kwa jamii ya Wahdzabe na waberbeig lakini pia vyanzo vya maji vitahifadhiwa"alisema
Clara Chuwa mratibu miradi wa Shirika la WODSTA alisema wanakwenda kutekeleza Mradi kwa ajili kuwezesha kutunza mazingira na matumizi endelevu ya msitu na chanzo Cha maji kijiji Cha lemanda, Kata ya oldonyosambu,wilaya ya Arumeru.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la SECCA ,Esaya Yusufu alisema wanakwenda kutekeleza mradi wa upandaji miti na kuchimba kisima katika eneo la ikolojia ya serengeti.
Mfuko wa mazingira Duniani(GEF) ulianzishwa mwaka 1992 na umekuwa na miradi katika nchi 136 Duniani.
Orodha ya mashirika yaliyopita kutekeleza miradi ni hii
1. Tanzania Natural Resources Forum (TNRF)
2. Monduli Women Action Trend (MOWAT)
3. Guluka Kwalala Youth Environment Group
4. Development Concern (DECO)
5. Environment and Energy Tanzania (EET)
6. Young Environmentalist Tanzania Organization (YET)
7. Hope for All (HFA)
8. Network for Vulnerable Rescue Foundation (NVRF)
9. Foundation for empowering local community's Initiatives (FELOCI)
10. Nguvu Kazi community-based organization
11. Mlangali Development Association (MLADEA)
12. Community Distinguished and Environmental Conservation (CODECO)
13. Environment for People and Development (EPD)
14. Jumuiya ya Uhamasishaji Wakulima Kilimo cha Kisasa Zanzibar (JUWAKIZA)
15. Sustainable for environmental and climate change association (SECCA)
16. JUHIWAPOMA community-based organization - Makao Wildlife Management Area.
17. Pakaya Culture and Environmental Group (PCEG)
18. Southern Tanzania Elephant Program (STEP)
19. The Tanzania Association of Foresters (TAF) -Zone of Zanzibar
20. Empowerment of Marginalized Communities (E-MAC) Tanzania
21. Climate Action Network (CAN) Tanzania.
22. Bagamoyo Non-Government Organization Networking (BANGONET)
23. Women Development For Science And Technology Association (WODSTA)
24. Tanzania Landscapes Restoration Organization (TaLRO)
25. Afrinurture For Peoples’ Development (AFRIPEDO)
26. Society For Environmental Conservation And Poverty Alleviation (SECOPA)
27. Connecting Youth Connecting Tanzania
28. Disability Relief Services Tanzania (DRS Tanzania)
29. Global Conservation Society (GCS)
30. Arid Lands Resource Initiatives Development Organization (ALARI)
31. Environmental Conservation For Wildlife And Community Enterprise (ECOWICE)
32. Usevya Development Society (UDESO)
33. Mpingo Conservation & Development Initiative (MCDI)
34. Pastoral Livelihood Support And Empowerment Program (PALISEP)
35. Zanzibar Association Of The Disabled (UWZ)
36. Nyasa Environmental Restoration Initiative (NERI)
37. Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Nyang’oro Kaskazini (MJUMINYAK)
38. Maasai Pastoralist Development Organization (MPDO – LARETO)
39. Mtandao Wa Jamii Wa Usimamizi Wa Misitu Tanzania (MJUMITA).
40. Nyuki Mgazini
41. Media Aid For Indigenous And Pastoralists Community (MAIPAC)
42. East Mara Women Foundation
43. Tanzania Development Light Organization (TADELO)
44. Pemba Trees Conservation Organization (PETCO)
No comments:
Post a Comment