Na: Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
MTENDAJI mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesema mpango mkakati wa kuhakikisha hadi ifikapo mwaka 2025/2026 asilimia 85 ya mtandao wa barabara wa kilometa 144, 429, 077 wanaozihudumia ziweze kupitika misimu yote umewekwa.
Alisema hayo Aprili 4, 2024 mjini Morogoro wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tarura cha kuipitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo itawasilishwa bungeni mwezi ujao na Waziri mwenye dhamama.
Mhandisi Seff alisema, lengo kuu la mkakati huo ni kuhakikisha barabara hizo zinapitika wakati wote ili kuchangamsha uchumi na kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii na za kiuchumi kwa urahisi.
Alisema kwa sasa zaidi ya kilometa 100,000 za barabara ni za udongo na ndizo zenye shida kubwa zinaponyesha mvua hata kwa kwiango kidogo na kusababisha nchi nzima inakuwa kama imesimama.
Mhandisi Seff alisema asilimia 44 uliobakia barabara zake ndizo zenye mtandao uliokuwa mzuri zikiwemo barabara za lami kilometa zaidi ya 3,200 na barabara za changarawe zaidi ya kilometa 41,000 .
Mtendaji mkuu wa Wakala huyo alisema kufanyika kwa baraza hilo ni hatua ya kuwashirikisha wafanyakazi ili waweke michango yao kwenye bajeti hiyo.
“ Madhumini ya vikao hivi vya baraza ni kuwashirikisha watumishi katika uendeshaji wa taasisi na katika uboreshaji wa maslahi yao ili kuwezesha kufikia lengo letu “ alisema Mhandisi Seff.
Naye Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini na Kazi za Ujenzi (TAMICO),Paternus Rwechungura aliishauri Tarura hususani wahandisi na wataalamu wanaoshughulika na ujenzi wasisite kujinga na chama cha wajenzi ili washirikiane na wenzao wakiwemo wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika kubadirishana uzoefu wa sekta ya ujenz
Katibu mkuu huyo aliushauri Wakala huo uendelee kuziangalia na kukarabati barabara zilizopo vijijini na mijini ili kuwezesha utoaji wa huduma za usafiri na usafirishaji kuwa bora na wa kuaminika nyakati zote .
Kwa upande wake mwakilishi wa Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Tulia Msemwa, aliwashauri wajumbe wa baraza hilo kutoa maoni na mapendekezo yao katika bajeti hilo ili kuhakikisha wakala huo unafikia malengo , dhima na dira iliyojiwekea .
Msemwa ambaye ni Ofisa Elimu Kazi Mwandamizi kutoka Ofisi hiyo alisema Tarura imejiwekea mipango mbalimbali hasa kuboresha miundombinu ya barabara ambayo yataisaidia kutatua changamoto na kufikia kwenye ufanisi wenye tija na malengo mazima yaliyowekwa na Taifa.
No comments:
Post a Comment