Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
CHUO kikuu Cha Sokoine cha Kilimo(SUA) katika kuongeza ufanisi wa kazi zaidi baina ya wafanyakazi na viongozi wa idara zake kimetakiwa kujenga mahusiano, maadili mema na kuwa na jitihada kazini.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Christian Bwaya alisema hayo mkoani Morogoro katika mafunzo maalumu kwa watumushi wa chuo hicho ya siku tatu ambapo alikuwa akitoa mada ya uongozi na maadili.
Bwaya alisema katika jitihada za kujenga madili mema kwa viongozi wa taasisi pamoja na wafanyakazi wake kwa kuleta chachu ya utendaji wa kazi chuoni hapo ni vyema kukawa na ushirikiano wenye kuleta tija kwa na Chuo kwa ujumla.
Aidha alisema kuwa mahusiano binafsi yanaweza kuchangia mmomonyoko wa maadili endapo mtumishi atatumia vibaya nafasi yake ya uongozi na kusababisha migogoro katika taasisi, hivyo akawataka watumishi katika taasisi hiyo kuwa kipaumbele katika kuhamasisha amani baina yao na kuheshimu kila ngazi ya uongozi kwa kila mtumishi.
"Kiongozi mzuri unatakiwa kuheshimu hisia zako mbele za wale unaowaongoza kuna mambo matano ya kuzingatia ikiwemo kujitambua binafsi, kumudu hisia, hamasa ya kufanya kazi, upendo na kuwa na nguvu ya kusikiliza ili kumpa uhuru mtumishi anayeongozwa kujiona anasikilizwa."alisema Bwaya.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo,mkurugenzi menejimenti ya rasilimali watu na utawala katika chuo kikuu cha SUA Peter Mwakilumwa alisema sababu ya kuandaa mafunzo ni kutimiza takwa la kisheria katika kutoa mafunzo Mara baada ya kuwa na uongozi mpya ili kutoa muongozo namna ya ufanyajikazi pasi na kukiuka taratibu na sheria za nchi.
"Suala la uongozi na kuwapa uwezo wa namna ya kukabiliana na changamoto ya uongozi pindi inapojitokeza tumeona ni muhimu kwetu sote naimani litaketa ufanisi na tija,"alisema..
Pia atoa wito wa washiriki wa mafunzo hayo kuyaishi na kuyatendea kazi yale yote yaliyofundishwa ili kujenga taasisi yenye uadilifu katika utendaji kazi na uongozi kwa ujumla.
Naibu makamu mkuu wa chuo SUA, mipango, fedha na utawala profesa Amandus Muhairwa alisemq afya na akili ya hisia kuwa chanzo cha kuathiri utendaji Wa kazi hasa kwa viongozi wa wafanyakazi hivyo elimu iliyotolewa itasaidia kutoa muongozo wa namna ya kutambua hisia za wafanyakazi wengine na namna ya kuendana nao kwa wakati sahihi.
"Kama mnavyoona licha ya kujifunza namna ya uongozi na mbinu za kuongoza afya ya akili na akili ya hisia kwa Kawaida ni vitu vinavyoathiri utendaji wa kazi kwa viongozi walio wengi na ndio sababu ya taasisi yetu kuandaa mafunzo haya ili kutoathiri ufanyaji wa kazi kwa weledi,"alisema Profesq Amandus.
Mmoja wa washiriki kwenye mafunzo hayo Gaymary George alisema kutokana na mafunzo hayo wanaamini kuwa watayatendea kazi pamoja na kukiri kuwa yatawasaidia kwenye uongozi wao kwani wametambua namna ya kuzungumza na watumishi pamoja na kulinda muonekano hasa mavazi na hii itaepusha tafsiri mbaya Kwa wanaowaongoza.
Mafunzo hayo yameendeshwa kwa viongozi kutoka taasisi mbalimbali na Kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua huku ikiwa ni taratibu ya chuo hicho kuandaa mafunzo maalum kwa ajili ya viongozi wa watumishi mbalimbali chuoni hapo mara baada ya kuteua viongozi wapya na kuwasaidia kutambua nafasi zao katika kufanya kazi kwa weledik na ufanisi zaidi.
No comments:
Post a Comment