SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MKAZO WA KUWAONDOA VIJANA KWENYE URAIBU WA DAWA ZA KULEVYA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 30 June 2024

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MKAZO WA KUWAONDOA VIJANA KWENYE URAIBU WA DAWA ZA KULEVYA

 




Na Mwandishi Wetu maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali inaendelea kuweka nguvu katika kuondoa vijana kwenye uraibu wa dawa za kulevya kwa kuhakikisha inawapa tiba ili warudi katika hali zao za kawaida.


Kauli hiyo ameitoa tarehe 29 Juni, 2024 wakati alipotembelea Mabanda ya Taasisi mbalimbali kuelekea Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Dunia 2024 zinazofanyika Jijini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana.


"Tumeshuhudia vijana wengi waliotoka kwenye uraibu wa dawa za kulevya wamerudi kuwa rai wazuri wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji mali na wameamua kujitokea kuokoa vijana wenzao," alisema Waziri Mhagama


“serikali imeshajenga kituo Jijini Dodoma cha urekebishaji ambacho kitakuwa kinatoa tiba ya kutoa vijana kwenye uraibu wa dawa za kulevya na kufundisha mafunzo ya ujuzi.” amefafanua


Aidha ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza kwa nguvu kubwa kwenye matamko ya kisera ili kuweza kuhakikisha inaokoa vijana kwenye matumizi ya dawa za kulevya.


Waziri Mhagama amesema pia kwa tafiti zilizofanyika mtumiaji akitumia dawa za kulevya anatumia masaa sita kwa kilevi ambacho kinamsababishia, jambo ambalo linamnyima uwezo wa kufanya kazi, hivyo kukosa fedha ya kununua madawa kunakomsababisha kuingia kwenye matendo ya jinai.


Awali Katika zoezi hilo Waziri Mhagama aliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi.

No comments:

Post a Comment