MDAU WA MAENDELEO TAIKO KULUNJU ATEMBELEA WATOTO WA LIGHT IN AFRICA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 8 July 2024

MDAU WA MAENDELEO TAIKO KULUNJU ATEMBELEA WATOTO WA LIGHT IN AFRICA

  






Na Mwandishi wetu, Mirerani 


maipacarusha20@gmail.com 


MDAU wa maendeleo wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Kulunju Oletipa akiwa na marafiki zake ametembelea kituo cha watoto yatima na waliokuwa wanaishi kwenye mazingira magumu wa Light In Africa na kutoa msaada wa vitu vyenye thamani ya shilingi milioni moja.


Taiko ametoa msaada huo kwenye kituo hicho wa vyakula ikiwemo mchele, maharage, tambi, sukari, mafuta ya kupikia, majani ya chai, witta bixs, mafuta ya kujipaka, blue band, sabuni na pampas.


Amesema ametoa msaada wa thamani ya shilingi milioni moja kwani vyakula hivyo bi vya thamani ya shilingi laki tano na kukabidhi shilingi laki tano taslimu.


"Tumeona zawadi hii kwao ili kile ambacho tunakipata kwenye shughuli zetu tule na watoto hawa nao wafurahi katika kituo hicho," amesema Taiko.


Ametoa wito kwa jamii na wadau wengine wa maendeleo kuwa na moyo wa kusaidia wahitaji kwa kile walichojaliwa na Mungu.


Hata hivyo, amewapongeza watumishi wa kituo cha Light In Africa kwa namna wanavyowahudumia na kuwasimamia watoto waliopo kwenye kituo hicho.


Msimamizi wa kituo hicho, Mary Moria amemshukuru Taiko kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika kama ulivyokusudiwa kwa watoto hao.


"Tunamshukuru Mungu kwa matoleo haya ambayo kwa namna moja au nyjngine itawasaidia watoto hawa wakiwemo walemavu," amesema Mary.


No comments: