MVOMERO KUENDESHA DORIA KUDHIBITI MIFUGO INAYOINGIA SHAMBANI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 22 July 2024

MVOMERO KUENDESHA DORIA KUDHIBITI MIFUGO INAYOINGIA SHAMBANI








Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com 


SERIKALI wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na jeshi la polisi wilayani humo imeweka mkakati wa kuendesha doria usiku ili kudhibiti mifugo inayochungwa kwenye mashamba ya wakulima na kuwasababishia hasara kubwa.


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli alitoa rai hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari kufuatia tukio la mfugaji mmoja aliyefahamika kwa jina la Taifa China kuachia mifugo yake majira ya usiku wa julai 21,2024 na kuingia kwenye mashamba ya wakulima yenye mazao ya mahindi na mpunga, lililopo eneo la Dakawa wilayani humo.


Nguli alisema ya kuwa kitendo cha wafugaji kutothibiti mifugo yao na kuiachia ikizagaa kwenye mashamba ya wakulima nyakati za usiku hakikubaliki kwa kuwa siyo kiashiria cha uwepo kwa utu kwa wafugaji wenye tabia ya aina hiyo.


Alisema ya kuwa, serikali imekuja na mkakati huo wa kufanya doria ya kusaka mifugo inayorandaranda nyakati za usiku  kwamba itakayokamatwa, sanjari na kuwasilishwa kwa ombi maalum mahakamani la kutoa kibali cha  kutaifishwa mifugo hiyo.


Maeneo yaliyoathiriwa na mifugo hiyo ni shamba la ushirika la wakulima wadogowadogo wa Mpunga skimu ya umwagiliaji Dakawa (UWAWAKUDA), Charles Pangapanga kwa kipindi kirefu walikuwa na changamoto za wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima, awali kulikuwa na maridhiano baina ya wakulima na wafugaji kwamba kila mmoja waheshimu maeneo ya mwenzake  kwa lengo la kudhibiti mifugo isiliingie kwenye mashamba ya wakulima.


Pangapanga alisema kuwa pamoja na maridhiano hayo,lakini wafugaji wamekuwa wakiuka na kuleta usumbufu mkubwa, mara kwa mara wamekuwa wakiingizaa mifugo kwenye shamba la ushirika lenye ukubwa wa ekari 5000 ambalo lina hati miliki na miundombinu ya skimu ya umwagiliaji na kusababisha hasara kwa wakulima.


Aliomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga ukuta kuzunguka eneo la shamba la ushirika ili kutafuta suluhisho la kudumu la kudhibiti mifugo kwa kuwa eneo hilo limewekwa miundombinu ya umwagiliaji kwa gharama kubwa.


Alisema kuwa baadhi ya wanaushirika wameingia mkopo kwenye taasisi za fedha kwa lengo la kuendesha kilimo cha kisasa lakini kwa hali ilivyo sasa wameingiwa na hofu ya kupata hasara na kushindwa kurejesha mkopo kutokana na uharibifu unayofanywa na mifugo inayochungwa kiholela.


Mbali na shamba la ushirika kuharibiwa na mifugo, Seleman Nassoro na Christina Juma wakulima wa Dakawa wameelezea changamoto za mifugo kuingia kwenye mashamba yao ya mpunga na mahindi na kuwasababishia hasara kubwa.


Christina alisema kuwa shamba lake la mahindi lenye ukubwa wa ekari moja limeharibiwa na mifugo hali ambayo inamfanya awe na hofu ya kutokuwa na chakula cha kutosha kwenye msimu huu.


Taifa china ni wafugaji mkazi wa Dakawa Wilayani Mvomero alipohojiwa na waandishi wa habari juu ya sakata hilo alisema mifugo yake ilivunja zizi na kuingia kwenye mashamba ya wakulima,lakini hawezi kujua hasara zilizosababishwa na mifugo yake.


Mwisho

No comments: