RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU SITA MKOANI MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 31 July 2024

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA SIKU SITA MKOANI MOROGORO

 



Na: Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku sita mkoani Morogoro ambapo atakagua miradi ya maendeleo 14.


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima alieleza hayo wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mkoani hapa.


Malima aliwaomba wananchi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi wakati wa ziara hiyo ya Rais Samia Suluhu Hassan hasa kwenye maeneo yote yaliyopangwa ambayo atapita au kusimama kuzungumza nao.


"Mimi kama mkuu wenu wa mkoa wa Morogoro niwaombe wakazi na wadau tuitikie kwa wingi na kujari heshima na mapenzi aliyotupatia kuja mkoani kwetu Morogoro.


Mkuu huyo wa mkoa alisema ziara hiyo itaanza Agosti 2 hadi 7,kwa Wilaya ya Gairo ambapo atakagua mradi wa Hospitali ya Wilaya na kuzungumza na wananchi, baadae kukagua miradi ya wakala wa barabara nchini(TANROADS), na Wakala wa Barabara Vijijini na mijini (TARURA) na kuja Hadi Dumila Wilaya ya Kilosa ambapo atazungumza na wananchi wa maeneo hayo.


Alisema , Rais Samia atakagua miradi ya sekta ya uzalishaji wa viwanda, umwagiliaji pamoja na kushiriki kwenye uanzishwaji wa mradi wa Tutunzane ambao unalengo la kutengeneza mazingira ya kupata amani, na kupata taarifa ya miradi mingine ya sekta ya mifugo.


Aidha mkuu huyo alisema Rais Samia atafungua Kiwanda kipya cha kuzalisha Sukari Cha Mkulazi na kufungua barabara ya Dumila, Rudewa Kwenda Kilosa yenye kilometa zaidi ya 70 ambayo Ina madaraja matatu makubwa.


Malima alisema miradi mingine itakaguliwa katika Wilaya ya Kilombero, na baadae Agosti sita atakagua Uwanja wa Jamhuri

No comments: