WATUMISHI KIBAHA MJINI WAWAFARIJI WATOTO WANAOLELEWA KWENYE VITUO YATIMA TISA, WATOA MISAADA YA MILIONI 40 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 7 July 2024

WATUMISHI KIBAHA MJINI WAWAFARIJI WATOTO WANAOLELEWA KWENYE VITUO YATIMA TISA, WATOA MISAADA YA MILIONI 40

 




Na: Julieth Mkireri, KIBAHA


maipacarusha20@gmail.com 


HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha imetoa misaada kwa watoto wanayoishi katika vituo vya kulelea watoto (makao) tisa yenye thamani ya sh. miln.40.

Mbali ya kutoa misaada hiyo watumishi, Madiwani na Viongozi wengine kutoka Halmashauri hiyo walijumuika na watoto kutoka katika vituo hivyo na kula nao chakula cha mchana.

Hiyo ni mara ya kwanza tangu Halmashauri hiyo ianzishwe  kwa watumishi wakiongozwa na Mkurugenzi kujumuisha vituo vya kulelea watoto na kuwapatia misaada sambamba na kufanya hafla kama hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Rogers Shemwelekwa amesema baada ya kumaliza mwaka wa fedha watumishi walihamia kwa pamoja kujumuika na watoto hao kwa kuwapatia misaada na kula nao chakula.

Amesema wamefanya hivyo kuwafariji watoto hao wasijione wapweke kwa kukosa baadhi ya vitu kwani vituo vingi vinategemea kupata misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa elimu bure na kuwawezesha watoto wanapotoka katika mazingira magumu kusoma bila vikwazo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amempongeza Mkurugenzi kwa kufanikisha jambo hilo ambalo limeleta faraja kwa watoto na wasimamizi wa vituo hivyo.

Lilian Mbise ni Mkurugenzi katika Kituo cha Shalom kilichopo Msangani amemshukuru Mkurugenzi, Watumishi, Mwenyekiti wa Halmashauri na Madiwani kwa kufanya hafla hiyo ambavyo imetumika kuwapatia misaada mbalimbali inayokwenda kusaidia watoto hao.


No comments: